• HABARI MPYA

  Saturday, December 06, 2014

  SAID BAHANUZI KWAHERI YANGA SC, ATUA JESHINI KWA MKOPO

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  YANGA SC imemtoa kwa mkopo mshambuliaji Said Rashid Bahanuzi ‘Spider Man’ katika klabu ya Polisi Morogoro.
  Bahanuzi amechagua kwenda Polisi badala ya timu zote zilizokuwa zikimuhitaji, Stand United na Ruvu Shooting kwa kuwa anaamini huko ni sehemu sahihi kwenda kufufua makali yake.
  Mshambuliaji huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar amejikuta katika wakati mgumu Yanga SC, baada ya kung’ara kwa msimu mmoja tu, 2012.
  Bahanuzi aliingia kwa kishindo Yanga SC akiiwezesha timu hiyo kutwaa Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kagame la Kagame 2012 naye pia kuwa mfungaji bora.
  Said Bahanuzi anakwenda kwa mkopo Polisi Morogoro

  Baada ya hapo, Bahanuzi akaanza vizuri pia kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kabla ya kuumia katikati ya msimu na kuwa nje hadi msimu uliofuata.
  Hata hivyo, tangu kuumia Bahanuzi hajaweza kurejea katika kiwango chake licha ya makocha wote aliofanya nao kazi Yanga SC baada ya Mbelgiji Tom Saintfiet kumpa nafasi.
  Hao ni Waholanzi Ernie Brandts na Hans van der Pluijm pamoja na huyu wa sasa, Mbrazil Marcio Maximo.  
  Tangu amejiunga Yanga SC, Said Bahanuzi amecheza mechi 48 na kufunga mabao 15, matatu kwa penalti.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAID BAHANUZI KWAHERI YANGA SC, ATUA JESHINI KWA MKOPO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top