• HABARI MPYA

  Saturday, December 06, 2014

  KIIZA AING’ARISHA YANGA, YAICHAPA 1-0 EXPRESS ILIYOIHENYESHA SIMBA JANA

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  BAO pekee la Hamisi Kiiza ‘Diego’ limeipa Yanga SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Express ‘Tai Wekundu’ ya Uganda katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni hii.
  Kiiza alifunga bao hilo dakika ya 90 na ushei akimalizia pasi ya Simon Msuva baada ya kutokea benchi kuchukua nafasi ya Haruna Niyonzima kipindi cha pili.
  Yanga SC ilicheza vizuri kipindi cha kwanza, lakini ilishindwa kutumia nafasi nyingi ilizotengeneza na kocha Marcio Maximo alimpumzisha Jerry tegete baada ya dakika ya 30, nafasi yake akiingia Mrisho Ngassa. 
  Wachezaji wa Yanga SC wakimpongeza Kiiza baada ya kufunga bao pekee la ushindi

  Kiungo mpya aliyesajiliwa kutoka Brazil, Emerson de Oliviera Roque hakuwepo hata benchi, ingawa mashabiki wengi walifika uwanjani leo kwa ajili ya kumuona. 
  Kasi ya mashambulizi ya Yanga SC iliongezeka zaidi kipindi cha pili, Ngassa akicheza pamoja na Niyonzima, baadaye Kiiza, Nizar Khalfan na Msuva, lakini wana Jangwani hao bahati yao iliishia kwenye bao moja.
  Express jana ilitoka sare ya 0-0 na Simba SC iliyowakosa wachezaji wawili nyota Waganda, Joseph Owino na Emmanuel Okwi. 
  Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mbuyu Twite, Said Juma ‘Kizota’/Salum Telela, Haruna Niyonzima/Kiiza, Jerry Tegete/Mrisho Ngassa, Simon Msuva na Andrey Coutinho/Nizar Khalfan.
  Express; Ali Kigundu, Kayiwa Ibrahim, Hassan Wasswa, Henri Katongile, Bob Kasozi, Ivan Sserunkuma, Thadeo Lwanga, Willy Kavuma, Mukasa Mussa, Simon Sserunkuma na John Semazi.  
  Nahodha wa Yanga SC, Nadir Haroub 'Cannavaro' akipambana na mchezaji wa Express
  Beki Oscar Joshua wa Yanga SC akimhadaa mchezaji wa Express
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIIZA AING’ARISHA YANGA, YAICHAPA 1-0 EXPRESS ILIYOIHENYESHA SIMBA JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top