• HABARI MPYA

  Monday, December 15, 2014

  RONALDO APIGA TUZO NYINGINE, MESSI MBONA ATAKUFA NACHO!

  TUZO nyingine imedondoka kwenye anga za Cristiano Ronaldo, baada ya Mwanasoka huyo Bora wa Dunia kushinda tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Mwaka wa Shirika la Utangazaji Tanzania (BBC).
  Katika sherehe za utoaji wa tuzo hizo mjini Glasgow, Scotland Ronaldo alishindwa kuhudhuria kwa sababu alikuwa Morocco, ambako timu yake, Real Madrid imeweka kambi.
  Lakini Mreno huyo akashiriki tuzo hizo kwa kupitia video na mchezaji mwenzake wa Real, Gareth Bale ndiye aliyemkabidhi tuzo Ronaldo nchini Morocco ambako wanajiandaa na Klabu Bingwa ya Dunia.
  Hii ni sababu nyingine ya Ronaldo kutembea kifua mbele dhidi ya mpinzani wake mkubwa, Lionel Messi wa Barcelona na Argentina.
  Cristiano Ronaldo holds his Overseas Sports Personality of the Year Award on Sunday night
  Cristiano Ronaldo akiwa ameshika tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Mwaka ya BB jana
  Ronaldo's Real Madrid team-mate Gareth Bale (left) presented him with the award in Morocco
  Ronaldo akikabidhiwa tuzo na mchezaji mwenzake wa Real Madrid, Gareth Bale (kushoto)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO APIGA TUZO NYINGINE, MESSI MBONA ATAKUFA NACHO! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top