• HABARI MPYA

    Monday, December 15, 2014

    HAMMILTON ASHINDA TUZO YA BBC

    BRAZAMENI Lewis Hamilton ameibuka dereva wa kwanza wa F1 tangu Damon Hill mwaka 1996 kushinda Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Mwaka wa Shirika la Utangazaji la BBC.
    Hamilton alishika nafasi ya pili mara mbili, mwaka 2007 na 2008 kabla ya kung’ara mwaka huu, akiwagaragaza Rory McIlroy aliyekuwa wa pili na Mwanariadha Jo Pavey wa tatu.
    Hamilton alipata kura 209,920 ambayo ni sawa na asilimia 33 ya kura zote, huku mcheza Gofu namba moja duniani, McIlroy akipata kura 123,745 sawa na asilimia 19.9.
    Timu ya wanawake ya Rugby England imeshinda tuzo ya Timu Bora ya Mwaka wakati, Sir Chris Hoy alipokea tuzo ya Mafanikio ya Muda Mrefu, huku nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ndiye Mwanamichezo Bora wa Jumla wa Mwaka.
    Hamilton (centre) poses alongside runner-up Rory McIlroy (right) and athlete Jo Pavey
    Hamilton (katikati) akiwa amepozi na mshindi wa pili Rory McIlroy (kulia) na Mwanariadha Jo Pavey

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/formulaone/article-2873462/Lewis-Hamilton-wins-BBC-Sports-Personality-Year-beating-Rory-McIlroy-crown.html#ixzz3Lw58G661 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HAMMILTON ASHINDA TUZO YA BBC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top