• HABARI MPYA

  Tuesday, December 16, 2014

  PIGO COASTAL UNION, KOCHA WAO YUSUF CJIPPO ATIMKIA AFC LEOPARDS

  Na Vincent Malouda, NAIROBI
  KOCHA wa Coastal Union Yusuf Kyenzi Chippo amejiunga na klabu ya AFC Leopards ya Kenya kama naibu kocha.
  Mkufunzi huyo wa zamani wa klabu ya Nzoia Sugar na timu ya taifa la Kenya Harambee Stars amempiku aliyekuwa kocha wa zamani wa vilabu vya Ulinzi Stars, Sofapaka na Mathare United Salim Ali ili kuwahi kazi hiyo.
  “AFC Leopards SC imethibitisha usajili wa Yusuf Kyenzi Chippo kama naibu kocha mpya. Kocha huyo mwenye cheti cha ukufunzi cha CAF ‘A’ anajiunga na klabu kutoka Coastal Union ya Tanzania”, ilisomwa taarifa kwenye mtandao wa Ingwe.
  Yusuf Chippo amewakimbia Coastal na kutua AFC Leopard ya kwao, Kenya

  Chippo anachukua nafasi yake Juma Abdallah ambaye alionyeshwa mlango baada ya msimu jana na anajiunga na kocha mpya wa walindamlango Idd Mohammed Salim aliyechukua nafasi yake Washingtone Muhanji.
  Mholanzi Hendrik Pietter De Jongh angali kocha mkuu japo zipo tetesi kuwa huenda akaonyeshwa mlango hivi karibuni.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PIGO COASTAL UNION, KOCHA WAO YUSUF CJIPPO ATIMKIA AFC LEOPARDS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top