• HABARI MPYA

  Thursday, December 04, 2014

  NG'OMBE HAZEEKI NA MAINI, DROGBA AING'ARISHA CHELSEA

  CHELSEA imeendelea vyema na mawindo yake ya taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya England, kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tottenham Hotspur usiku huu Uwanja wa Stamford Bridge, London.
  Eden Hazard aliifungia Chelsea bao la kwanza dakika ya 19, akimtungua Hugo Lloris ndania ya boksi, kabla ya mkongwe Didier Drogba kufunga la pili dakika tatu baadaye.
  Gary Cahill alilazimika kutoka nje mapumziko baada ya kuumia kichwani kufuatia kugongana na Jan Vertonghen na Loic Remy akatokea benchi kuchukua nafasi ya Drogba na kuifungia Chgelsea bao la tatu 73.
  Matoeko haya ni muendelezo wa unyonge wa Tottenham kwenye himaya Chelsea, kwani Spurs hawajashinda Uwanja wa Stamford Bridge kwenye Ligi Kuu ya England kwa miaka 24 sasa. Didier Drogba gets ahead of Jan Vertonghen to put Chelsea two up just three minutes after Hazard's goal
  Didier Drogba akimtoka Jan Vertonghen kabla ya kuifungia Chelsea katika ushindi wa 3-0 usiku huu
  The irrepressible striker celebrates his goal by the corner flag and the match was as good as done
  Drogba akishangilia kwa staili yake maarufu Stamford Bridge

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2859615/Chelsea-3-0-Tottenham-Eden-Hazard-Didier-Drogba-Loic-Remy-lead-Blues-cruise.html#ixzz3KsMOKbvn
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NG'OMBE HAZEEKI NA MAINI, DROGBA AING'ARISHA CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top