• HABARI MPYA

  Thursday, December 04, 2014

  BABBI ASAINI MWAKA MMOJA MALAYSIA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  KIUNGO wa zamani wa Yanga SC, Abdi Kassim Sadallah ‘Babbi’ jana amesaini Mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kuichezea UiTM FC katika Ligi Kuu ya Malaysia.
  Awali, Babbi alitaka kuihama klabu hiyo ajiunge na Sabah pia ya Ligi Kuu ya Malaysia, lakini wakashindwana kimaslahi. “UiTM FC imekuwa timu yenye maslahi zaidi kwangu kuliko Sabah, hivyo nitakuwa nayo kwa msimu wa pili mfululizo,”amesema Babbi akizungumza kwa simu na BIN ZUBEIRY jana usiku.
  Babbi ambaye pia anafahamika kama Ballack wa Unguja, akifananishwa na kiungo wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani, Michael Ballack ndiye mchezaji wa kwanza kufunga bao katika Uwanja mpya wa Taifa, Dar es Salaam baada ya kufunguliwa mwaka 2007.
  Abdi Kassim kushoto akisaini Mkataba wa mwaka mmoja na Rais wa UiTM, Hiziwan Mohamed jana. Picha ya chini Babbi akiwa nyumbani kwake Malaysia usiku baada ya mazoezi

   

  Babbi alifunga bao hilo Septemba 1, mwaka 2007 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Uganda, The Cranes- enzi hizo Taifa Stars ikifundishwa na kocha Mbrazil, Marcio Maximo ambaye kwa sasa yupo Yanga SC.
  Babbi aliibukia Mlandege ya Zanzibar mwaka 2002 kabla ya 2004 kuhamia Mtibwa Sugar ya Morogoro ambako alidumu hadi 2007 aliponunuliwa na vigogo wa Tanzania, Yanga SC.
  Mwaka 2011 Babbi aliuzwa Dong Tam Long Anya Vietnam ambako alicheza hadi 2012  aliporejea nyumbani kujiunga na Azam FC. 
  Mwaka 2013, Babbi alikwenda KMKM kabla ya mapema mwaka huu kujiunga na UiTM FC ambayo anaingia nayo katika mwaka wa pili sasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BABBI ASAINI MWAKA MMOJA MALAYSIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top