• HABARI MPYA

  Sunday, December 14, 2014

  MAN UNITED 'CHUMA CHIKOLI MOTO', LIVERPOOL YABAMIZWA 3-0

  MANCHESTER United imeshinda mechi ya sita mfululizo katika Ligi Kuu ya England, kufuatia kuichapa mabao 3-0 Liverpool Uwanja wa Old Trafford jioni ya leo.
  Ushindi huo, unaipeleka United nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu England kwa kutimiza pointi 31, ikizidiwa tano na Manchester City walio nafasi ya pili.
  Nahodha wa Mashetani hao Wekundu, Wayne Rooney alifunga sherehe za mabao dakika ya 12 akimalizia kazi nzuri ya winga Antonio Valencia aliyewatoka mabeki wa Liverpool. 
  Rooney alifunga bao hilo kiasi cha sekunde 25 baada ya Raheem Sterling kukosa bao la wazi upande wa Liverpool, kabla ya Juan Mata kufunga la pili dakika ya 40 akimalizia kazi ya Robin van Persie.
  Mshambuliaji wa Uholanzi, Van Persie akahitimisha ushindi wa timu ya Louis Van Gaal kwa bao la tatu dakika ya 71 akimalizia pasi ya Mata.
  Manchester United; De Gea, Valencia, Jones, Evans, Young, Carrick, Fellaini, Mata, Rooney/Falcao dk77, Van Persie na Wilson/Herrera dk71.
  Liverpool; Jones, Skrtel, Johnson/Toure dk25, Lovren, Moreno/Markovic dk68, Henderson, Allen, Gerrard, Coutinho, Lallana/Balotelli dk46 na Sterling.
  Wayne Rooney slides in to join his fellow goalscorers Juan Mata and Robin van Persie after the latter finished off their third against Liverpool
  Wayne Rooney akiteleza kwa magoti kuungana na wafungaji wenzake leo, Juan Mata na Robin van Persie baada ya bao la tatu
  Marouane Fellaini is outpaced by Adam Lallana and finds himself in referee Martin Atkinson's book after this challenge
  Marouane Fellaini akiondosha mpira miguuni mwa Adam Lallana 

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2873494/Manchester-United-3-0-Liverpool-Raheem-Sterling-misses-Wayne-Rooney-hits-25-seconds-later-misery-heaped-Reds.html#ixzz3LtA88dnA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED 'CHUMA CHIKOLI MOTO', LIVERPOOL YABAMIZWA 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top