• HABARI MPYA

  Friday, December 19, 2014

  KUMEKUCHA BEACH BAND BONANZA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BENDI mbalimbali za muziki wa dansi pamoja na wasanii wa Bongo Fleva wanatarajia kushiriki katika bonanza kubwa la burudani liitwalo ‘Beach Band Bonanza’ litakalofanyika kesho katika Ufukwe wa Azura, uliopo Kawe jijini Dar es Salaam.
  Akizungumza na waandishi wa habari jana, Msemaji wa Team Mamba ambao ni waratibu wa bonanza hilo Doris Godfrey alisema bonanza hilo litashirikisha bendi mbalimbali za dansi zikiwemo FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, Sky Light, Mapacha Watatu, wasanii wa Bongo Fleva akiwemo Dully Sykes, CPWAA na kundi la Yamoto Band.

  “Napenda kuwakaribisha katika bonanza hili, tutachanganya ladha tofauti ili kuvutia kwa kujumuishaBongo Fleva na Dansi, kiingilio kitakuwa Sh 10, 000 na watoto Sh 5, 000, tunatarajia kuanza saa sita mchana na pia kutakuwa na michezo mbalimnbali ya watoto,” alisema.
  Kwa upande wake Rais wa FM Academia, Nyoshi El Saadat alisema wanatarajia kuporomosha burudani ya aina yake katika bonanza hilo.
  Kwa upande wao wadhamini wa bonanza hilo, Kampuni ya Mabibo Beer chini ya bia yao ya Windhoek, Meneja Biashara wa kampuni hiyo,    Joseph Boniface, alisema bonanza hilo ni la aina yake na wao wameona kuwakutanisha bendi za muziki wa Dansi na Bongo Fleva ili kuwapa mashabiki burudani ya aina yake.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KUMEKUCHA BEACH BAND BONANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top