• HABARI MPYA

  Friday, December 19, 2014

  KIBADENI AREJESHWA SIMBA SC

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  MCHEZAJI na kocha wa zamani wa Simba SC, Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ amerejshwa katika klabu hiyo.
  Kibadeni mwenye rekodi ya mchezaji pekee kufunga mabao matatu katika katika mechi moja dhidi ya watani, Yanga safari harudi Simba kama kocha wala mchezaji, bali amepewa uonbgozi.
  Rais wa Simba SC, Evans Eliza Aveva leo ametaja Kamati ndogo ndogo ndani ya klabu hiyo na Kibaden amepewa Umakamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi, chini ya Mwenyekiti Collin Frisch. Wajumbe wa Kamati hiyo ni Mohamed Yakob, Patrick Rweyemamu, Othman Kazi, Geiorge Lucas na Duwa Said.
  Abdallah Kibaden kushoto amerejeshwa Simba SC kama Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi

  Kapteni wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Zacharia Hans Poppe ataendelea kuongoza Kamati ya Usajili, Makamu wake akiwa ni Kassim Mohammed Dewji na Wajumbe Crescentius John Magori, Said Tulliy, Collin Frisch, Musleh Al-Rawahi na Rodney Chiduo.
  Kamati ya Mashindano Mwenyekiti ni Mohamed Nassoro ‘Steven Seagal’, Makamu wake Idd Kajuna na Wajumbe Gerald Yambi, Hamphrey Mkumbo, Bituro Kazeri, Juma Ndambile, Hemed Milanzi na Abdul Salehe. 
  Kamati ya Soka la Vijana Mwenyekiti ni Said Tulliy, Makamu wake Juma Pinto Wajumbe na Wajumbe Amina Poyo, Mulamu Nghambi, Juma Ndambile, David Kivembele, Hemed Omary na Rehule Nyaulawa.
  Kamati ya Fedha Mwenyekiti: Geofrey Nyange 'Kaburu', ambaye pia ni Makamu wa Rais wa klabu, Makamu Aziz Kefile na Wajumbe Jasmine Badouh, Muhada Engbert, Nicky Magarinzi, Mchalange France na Ally Suru.
  Kamati ya Maadili Mwenyekiti ni Samson Mbamba, Makamu Hassan Tikka na Wajumbe Peter Muinzi, Gerlad Mongella na Hassan Mnyenye.
  Kamati ya Nidhamu Mwenyekiti ni Michale Ngallo,
  Makamu Said Hemed El Maamry na Wajumbe Fotonatus John Mangwela. Ismail Mohamed na Ngasa Ganja, wakati Kamati ya Masoko Mwenyekiti ni Salim Abdallah ‘Try Again’, 
  Makamu wake Crescentus Magori na Wajumbe Azim Dewji, Musleh Al Rawahi, Iman Kajula, Juma Pinto, Farough Baghoza na Ruge Mutahaba.
  Kamati ya Wanachama na Matawi Mwenyekiti wake Kassim Dewji, Makamu Idd Kajuna na Wajumbe: Mulamu Ngh'ambi, Masoud Hassan, Abdul Mshangama, Omary Mkonje, Albino Lwila, Hassan Mkande, Hussein Simba, Yahaya Athuman, Hassan Kaniki, Bakary Ngurumo, Seydou Rubei, Manesh Rupareria, Omary Makamba, Omary Makoye, Said Kubenea, Shaaban Nyaa, Abdulkarim Juma, Msumari Mbwana, John Bondo na Bakary Mnyachi.
  Aveva pia ametaja Kamati ya Muda ya Matamasha ya klabu chini ya Mwenyekiti Gerald Yambi, Makamu Mulamu Ngh'ambi na Wajumbe Dk Mohammed Wandi, Jasmine Badour, Said Nembo, Peter Richard na Ramadhan Hamisi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIBADENI AREJESHWA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top