• HABARI MPYA

  Friday, December 19, 2014

  KIPA MGANDA ATUPIWA VIRAGO SONY SUGAR

  Na Vincent Malouda, NAIROBI
  HUKU vilabu vya ligi kuu ya taifa la Kenya vikijiandaa kumenyana msimu ujao, vingi vimeanza harakati za kuwatema wachezaji ambao hawakufanya vema katika msimu wa 2014 uliyokamilika mwezi Novemba mwaka huu.
  Klabu ya SoNy Sugar haijaachwa mbali baada ya kuwapiga shoka watano akiwemo mzawa wa Uganda na mlindamlango Ronny Kagunzi (pichani juu) aliyejiunga nao mwezi Juni 2014 kutokea Top Fry AllStars zamani akiipigia ngoma Nairobi City Stars.
  Golikipa Joseck Gathongo pia hajaachwa nje sawia na beki Antony Odinga na washambulizi Andrew Antony na Patrick Kennedy Otieno maarufu kama ‘Agogo’.
  ‘Agogo’ hata hivyo alisitisha mkataba wake ili kurejea Thika United alikotoka mwezi Juni 2014.
  Wanasukari hao waliyoko magharibi mwa Kenya mjini Awendo walimaliza nambari tisa kwenye jedwali la timu 16 kwa alama 38 baada ya mechi 29 kwani hawajacheza ya mwisho dhidi ya AFC Leopards kutokana na vuta nikuvute kati ya Shirikisho la Soka la Kenya, FKF, na wasimamizi wa ligi kuu ya taifa la Kenya, KPL.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIPA MGANDA ATUPIWA VIRAGO SONY SUGAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top