• HABARI MPYA

  Friday, December 19, 2014

  BOBAN, MAFTAH KUTAMBULISHWA KESHO FRIENDS RANGERS

  Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WACHEZAJI wa zamani wa Simba SC, beki Amir Maftah na kiungo Haruna Moshi ‘Boban’ wanatarajiwa kutambulishwa rasmi kesho katika timu yao mpya, Friendsa Rangers ya Daraja la Kwanza.
  Rangers kesho inajitupa kwenye Uwanja wa Makurumla, Magomeni Mwembechai, kuvaana na timu ya Ndanda FC ya Mtwara, katika mchezo wa kirafiki wa kijaindaa na mzunguko wa pili wa ligi daraja la kwanza.
  Ofisa habari wa timu hiyo Asha Kigundula, alisema kikosi hicho kinashuka dimbani kikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi hiyo inayoanza kutimua vumbi Ijumaa ya Desemba 26.
  Haruna Moshi 'Boban' atatambulishwa kesho Rangers

  Alisema kwa kutambua umuhimu wa michuano hiyo ambapo wao wataanzia ugenini dhidi ya Lipuli ya Iringa, imejipanga kupata mechi kadhaa za kirafiki, ambapo kesho Jumapili itakuwa na mchezo mwingine dhidi ya Ruvu Shooting.
  Kigundula alisema kuwa kikosi chao kipo katika maandalizi makali ya kuhakikisha  kinaendeleza rekodi yake ya kutofungwa kama ilivyokuwa katika mzunguko wa kwanza wa michuano hiyo.
  Alisema timu yao chini ya kocha wake Ally Yusuph 'Tigana' kimewasajili Haruna Moshi 'Boban' Amir Maftah, na Robert, wengine ambao wamekuja kwa mkopo Wine Abbas kutoka Ruvu Shooting na Mahamod Osman kutoka Coastal Union.
  "Tunaendelea kukinoa kikosi chetu kwa kupata mechi nyingi za kirafiki lengo letu ni kuendelea na safari yetu ya kupanda daraja, ambapo msimu ujao tunataka kucheza ligi kuu"alisema Kigundula.
  Friends Rangers inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi daraja la kwanza, huku Majimaji ikishika usukani wa ligi hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BOBAN, MAFTAH KUTAMBULISHWA KESHO FRIENDS RANGERS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top