• HABARI MPYA

  Monday, December 15, 2014

  AZAM FC YAMTUPIA VIRAGO STRAIKA MHAITI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Azam FC imemtema mshambuliaji wa kimataifa wa Haiti, Leonel Saint-Preux baada ya kushindwa kuvumilia nidhamu yake mbovu.
  Azam FC inaridhika na uwezo wa Leonel kiuchezaji, lakini nidhamu yake mbovu ambayo alikuwa amekwishaanza kuwaambukiza wachezaji wengine waadilifu wa klabu hiyo, inafanywa aachwe.
  Habari kutoka ndani ya Azam FC zinasema kwamba Leonel alikuwa mfano mbaya ndani ya kambi ya timu na alikwishaanza kuwaambukiza na wachezaji wengine tegemeo wa timu hiyo.
  Tayari Azam FC imekwishaziba pengo la Mhaiti huyo kwa kumsajili winga wa kimataifa wa Uganda, Brian Majwega.
  Leonel Saint-Preux kushoto wakati anakabidhiwa jezi ya Azam FC baada ya kusajiliwa Julai mwaka huu

  Winga huyo wa KCCA ya Kampala, Uganda alisaini Mkataba wa miaka miwili jana mjini Kampala, Uganda kujiunga na mabingwa hao wa Tanzania Bara.
  Majwega anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Azam FC katika dirisha dogo baada ya beki Serge Wawa Pascal kutoka Ivory Coast, aliyekuwa anacheza El Merreikh ya Sudan na Amri Kiemba aliyekuwa Simba SC, ambaye amesainiwa kwa mkopo hadi mwisho wa msimu.     
  Na anakamilisha idadi ya wachezaji watano wa kigeni, baada ya Mrundi Didier Kavumbangu na Kipre Tchetche, Kipre Balou na Serge Wawa wote kutoka Ivory Coast.
  Majwega anatarajiwa kuanza mazoezi na kikosi cha Azam FC leo mjini Kampala, chini ya makocha Mcameroon Joseph Marius Omog na Mganda George ‘Best’ Nsimbe ambacho kipo kambini mjini humo tangu Ijumaa hadi Desemba 22, mwaka huu.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAMTUPIA VIRAGO STRAIKA MHAITI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top