• HABARI MPYA

  Thursday, December 11, 2014

  FM ACADEMIA, YAMOTO, MAPACHA NA SKYLIGHT KUPAMBA BEACH BAND BONANZA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BENDI nne nyota jijini, FM Academia, Yamoto, Mapacha na SkyLight zitatumbuiza katika jukwaa moja kwenye tamasha la Beach Band Bonanza lililopangwa kufanyika Desemba 20 kwenye ufukwe wa Azura, Kawe  darajani.
  Bonanza hilo limeandaliwa na kampuni ya Team Mamba na mbali ya bendi hizo nyota, wasanii wa bongo fleva wakiongozwa na Dully Sykes, CPWAA na Damian Soul ambaye atakuja na bendi yake.
  Msemaji wa kampuni ya Team Mamba, Doris Godfrey alisema kuwa bonanza hilo lililodhaminiwa Coca-Cola na bia ya Windhoek, limepangwa kuanza saa 6 mchana mpaka alfajiri.

  Rais wa Bendi ya FM Academia, Nyoshi El Saadat akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jana kuhusu Beach Band Bonanza litakalofanyika Desemba 20 katika ufukwe wa Azura jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Ilunga Khalifa (Cpwaa) na Mratibu wa Bonanza hilo, Dorice Godfrey. 

  Doris alisema kuwa wameandaa bonanza hilo kwa ajili ya kuwakutanisha wadau wa muziki na familia zao kwani siku hiyo kutakuwa na michezo ya watoto mchana na baadaye usiku kwa ajili ya wakubwa.
  Alisema kuwa pia kutakuwa na michezo ya watoto, kupanda farasi na michezo mingine ambayo ni ya kuvutia.
  “Hili ni bonanza la kwanza la muziki linalokutanisha bendi nyingi ambazo zitafanya shoo katika jukwaa moja, hivyo tunatarajia kuwa na burudani aina yake kwani bongo fleva nao watakuwepo kwa lengo kutoa burudani safi,” alisema Doris.
  Kiongozi wa bendi ya FM Academia, Nyoshi El Sadaat alisema kuwa wamejiandaa vizuri kutoa burudani katika bonanza hilo la aina yake. “Tuna nyimbo mbalimbali mpya, staili mpya ambazo siku hiyo zitakuwa zinaonyeshwa mara kwanza jukwaani,” alisema Nyoshi.
  Kwa upande wake, Dully Sykes alisema kuwa wamejiandaa vilivyo kwa ajili ya tamasha hilo na kuwaomba mashabiki wa muziki kufika kwa wingi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FM ACADEMIA, YAMOTO, MAPACHA NA SKYLIGHT KUPAMBA BEACH BAND BONANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top