• HABARI MPYA

  Thursday, December 11, 2014

  CECAFA YAITISHA MKUTANO MKUU WA DHARULA

  Na Vincent Malouda, NAIROBI
  BARAZA la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati, CECAFA, limeandaa Mkutano Mkuu wa dharura mjini Nairobi, Kenya siku utakaofanyika Jumapili wiki hii.
  Mkutano huu umeitishwa na Mwenyekiti wa CECAFA, Leodegar Tenga na masuala mbalimbali yanatarajiwa kujadiliwa kuhusu mambo yanavyoendeshwa kwenye bodi hiyo pamoja na changamoto za kuandaa Kombe la Challenge mwaka huu.
  Kumekuwa na purukushani ya nani atakayeandaa mashindano ya mwaka huu baada ya wenyeji wa hapo awali Ethiopia kujiondoa kwa sababu binafsi huku juhudi za Katibu Mkuu, Nicholas Musonye kushawishi mataifa ya Sudan na Rwanda kuiandaa kugonga mwamba.
  Mwenyekiti wa CECAFA, Leodegar Tenga kushoto

  Hata hivyo, mkutano huo wa Jumapili utatanguliwa na ule wa Kamati ya Utendaji utakaofanyika Jumamosi katika afisi za CECAFA zilizopo Uwanja wa Taifa wa Nyayo mjini Nairobi, Kenya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CECAFA YAITISHA MKUTANO MKUU WA DHARULA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top