• HABARI MPYA

  Wednesday, December 10, 2014

  FIFA YAIWEKEA NGUMU BARCA KUSAJILI BEKI MWINGINE BAADA YA VERMAELEN KUUMIA

  FIFA imesema Barcelona haitapewa ruhusa maalum ya kusajili beki baada ya kuumia kwa Thomas Vermaelen ambaye anatakiwa kuwa nje kwa miezi kadhaa.
  Barcelona ilifikiri itapewa ruhusa maalum kwa mujibu wa sheria za Shirikisho la Soka Hispania licha ya kukabiliwa na adhabu ya mwaka mmoja ya FIFA kutosajili.
  FIFA imeiambia Barcelona juzi kwamba Kamati yake ya Nidhamu haitoa ruhusa yoyote ya kusajili nje utaratibu wa kawaida wa usajili uliowekwa.
  Thomas Vermaelen underwent surgery on a hamstring injury that will keep him out for several more months
  Thomas Vermaelen amekwenda kufanyiwa upasuaji ambao utamuweka nje kwa miezi kadhaa

  FIFA iliifungia Barcelona kwa kuvunja sheria za kimataifa za usajili wa wachezaji wadogo. Itaanza Januari na itategemea na rufaa yao waliokata Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo.
  Mbelgihi huyo aliyesajiliwa kutoka Arsenal kwa dau la Pauni Milioni 15 hajacheza tangu atue Camp Nou.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FIFA YAIWEKEA NGUMU BARCA KUSAJILI BEKI MWINGINE BAADA YA VERMAELEN KUUMIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top