• HABARI MPYA

  Tuesday, December 16, 2014

  CHIPOLOPOLO WADOGO WATWAA NDOO YA U20 COSAFA

  Na Mwandishi Wetu, BULAWAYO
  TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Zambia jana imeifunga Zimbabwe mabao 3-0 mjini Bulawayo na kutwaa Kombe la Cosafa.
  Young Chipolopolo ilianza na moto wake mwanzo mwisho kwenye mashindano hayo, ikifunga jumla ya mabao 19 baada ya kuichapa Afrika Kusini 6-1, Namibia 2-0, Lesotho 4-0 na Malawi 4-0 katika Nusu Fainali.
  Mabao yote matatu jana waliyapata kipindi cha pili kupitia kwa Patrick Ngoma, Harrison Chisala na Solomon Sakala.
  Zimbabwe pia wanapaswa kumshukuru kipa wao, Kelvin Shangiwa aliyeokoa michomo ya hatari ya kiungo Patson Daka mara mbili dakika ya 14 na 30.

  Ngoma aliifungia Zambia bao la kwanza dakika ya 53 akimalizia krosi ya Crispin Sakulanda, kabla ya Chisala kufunga la pili dakika nne baadaye akiunganisha krosi ya Charles Shezongo na Solomon Daka kuhitimisha ushindi huo dakika ya 77 kwa penalti bsaada ya Sakulanda kuangushwa na Leslie Lunga aliyetolewa kwa kadi nyekundu.
  Young Chipolopolo sasa itatetea taji hilo mwakani nyumbani wakati Zambia watakapokuwa wenyeji Desemba 2015.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHIPOLOPOLO WADOGO WATWAA NDOO YA U20 COSAFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top