• HABARI MPYA

  Thursday, December 11, 2014

  AROUNA KONE APANIA KUREJEA KWA KISHINDO KAZINI

  MSHAMBULIAJI Arouna Kone amepania kurejea kwa kishindo uwanjani baada ya miezi 15 ya kuwa nje kwa sababu ya majeruhi.
  Mpachika mabao huyo wa kimataifa wa Ivory Coast atacheza mechi yake ya kwanza Everton tangu Oktoba 19, mwaka 2013 wakati atakapoanza leo katika mechi ya Europa League dhidi ya Krasnodar ya Urusi.
  Kone, ambaye alinunuliwa kwa Pauni Milioni 6 kutoka Wigan, hajaifungia bao Everton kabla ya kuumia na kuwa nje kwa muda mrefu sasa. 
  Aroune Kone, akizungumza na Waandishi wa Habari kabla ya safari ya Everton kuwafuata Krasnodar

  KIKOSI CHA EVERTON KINACHOTARAJIWA KUANZA LEO 

  Mfumo wa 4-2-3-1: Robles; Hibbert, Alcaraz, Browning, Garbutt; Osman, Ledson; Pienaar, Barkley, Oviedo; Kone.
  Pamoja na kwamba Kone anafikisha miaka 31 sasa, yuko tayari kupambana kushindania namba dhidi ya Samuel Eto’o na Romelu Lukaku.
  "Kama nitaweza kufunga, itakuwa babu kubwa," amesema Kone. "Itakuwa salamu tosha sana kwa kurejea kwangu kwa kishindo. Nina hamu sana ya kufunga bao langu la kwanza Everton. Itakuwa raha,"amesema.
  Mshambuliaji huyo wa Ivory Coast hajaifungia bao Everton tangu ajiunge nayo mwaka 2013
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AROUNA KONE APANIA KUREJEA KWA KISHINDO KAZINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top