• HABARI MPYA

  Sunday, December 07, 2014

  AZAM VETERANS YATOA SARE 5-5 NA BANDARI MOMBASA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mganda, George ‘Best’ Nsimbe jana aliiongoza timu ya maveterani wa Azam FC kutoa sare ya 5-5 na Bandari ya Mombasa, Kenya katika mchezo wa kirafiki, uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Kocha huyo Msaidizi aliyeajiriwa Azam FC kutoka KCCA ya Kampala, aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya kocha wa Azam Academy, Idd Nassor ‘Cheche’, lakini akashindwa kuipa ushindi Veterans.
  Mshambuliaji tegemeo wa Azam Veterans na Nahodha, Abdulkarim Amin ‘Popat’ alifunga mabao mawili, wakati mengine yalifungwa na Mange Issa, Iddi Cheche na Hassan Mohamed.
  Wachezaji wa Bandari Mombasa wakiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wao, Azam Veterans jana Chamazi kabla ya mechi
  Nahodha wa Azam Veterans kushoto Karim Popat akisalimiana na Nahodha wa Bandari

  Maveterani wa Mombasa wao mabao yao yalifungwa na Hamisi Kafani mawili, Joseph Nyachwaya, Abdillahi Juma na Ali Msemo.
  Kikosi cha Azam Veterans kilikuwa; Ali Manji, Adam Juma, Omar Salum, Luckson Kakolaki, Ibrahim Shikanda, Iddi Cheche, Philip Alando, Nassor Idrisa ‘Father’, Abdulkarim Amin ‘Popat’, Mange Issa na Hamis Jaffar.
  Bandari Mombasa; Robert Mweli, Charles Musiko, Ali Daini, George Ouma, Yusuf Ali, Hamisi Kafani, Ali Msemo, Abdillahi Salim, Evans Andeso, Abdillah Juma na Joseph Nyachwaya chini ya kocha Patrick Wanyama.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM VETERANS YATOA SARE 5-5 NA BANDARI MOMBASA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top