• HABARI MPYA

  Sunday, December 07, 2014

  APR NA RAYON ZOTE ZAKUNG’UTWA NA KUTUPWA NJE YA MICHUANO KIGALI

  Na Mwandishi Wetu, KIGALI
  WAPINZANI wa jadi katika soka ya Rwanda, APR na Rayon Sports wote wamefungwa na AS Kigali na Police FC na kutolewa katika michuano ya Kombe la Ombudsman Uwanja wa Amahoro.
  Michuano hiyo iliyoshirikisha timu nne zilizoshika nafasi za juu, iliyoandaliwa ili kupiga vita rushwa Rwanda, imekuwa na msisimko wa aina yake.
  Katika mchezo wa kwanza, kiungo Yannick Mukunzi aliifungia APR bao la kuongoza mapema kipindi cha kwanza, lakini AS Kigali ikasawazisha kwa bao la kujifunga la beki wa kulia Michel Rusheshangoga.
  APR wametolewa kwa matuta Kombe la Ombudsman Uwanja wa Amahoro jana 

  Baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 90, mshindi aliamuliwa kwa mikwaju ya penalti na AS Kigali ilishinda 3-1 baada ya Bodo Ndikumana, Isaiah Songa na Rodriguez Murengezi wote kutumbukiza nyavuni mikwaju yao, licha ya Ernest Sugira kukosa.
  Wachezaji wa APR, Emery Bayisenge, Nahodha Ismael Nshutiyamagara na Djamal Mwiseneza wote walikosa penalti zao zilizookolewa na kipa Shamiru Batte wakati Patrick Sibomana ndiye pekee aliyefunga.
  Katika mchezo wa pili, Police iliichapa Rayon Sports mabao 2-1 na kuweka hai matumaini ya kutetea taji hilo ambao walilitwaa mwaka jana.
  Jimmy Mbaraga alifunga bao la kwanza dakika ya 15, lakini Rayon Sports wakasawazisha kupitia kwa Nahodha, Faustin Usengimana dakika ya 12 kabla ya bao la dakika za lala salama la Innocent Habyarimana kuipa ushindi Polisi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: APR NA RAYON ZOTE ZAKUNG’UTWA NA KUTUPWA NJE YA MICHUANO KIGALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top