• HABARI MPYA

  Sunday, December 07, 2014

  SIMBA SC ‘ROJO ROJO’, YATANDIKWA 4-2 NA MTIBWA SUGAR CHAMAZI LEO

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  WIKI moja, kabla ya kumenyana na mahasimu, Yanga SC katika mechi ya Nani Mtani Jembe, Simba SC leo imefumuliwa mabao 4-2 na Mtibwa Sugar katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Simba na Yanga zitamenyana na Jumamosi ijayo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mechi ya Nani Mtani Jembe 2- na leo kocha Mzambia Patrick Phiri ametoka kichwa cha chini kwa kipigo kikali.  
  Simba SC ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao, mfungaji kiungo Said Ndemla kabla ya Mussa Hassan Mgosi kuisawazishia Mtibwa Sugar dakika ya 28.
  Simba SC ilipata pigo dakika ya 45 baada ya Ndemla kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Pierre Kwizera.
  Kocha Patrick Phiri leo timu yake imefungwa mabao 4-2 na Mtibwa Sugar wiki moja kabla ya kumenyana na mahasimu, Yanga SC katika Nani Mtani Jembe 

  Kipindi cha pili, Mtibwa inayofundishwa na Nahodha wake wa zamani, Mecky Mexime ilifanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 51, ingawa alionekana kama aliupiga mpira mkononi mwa kipa Ivo Mapunda.
  Mohammed Ibrahim aliyeingia kuchukua nafasi ya Mgosi kipindi cha pili, aliifungia Mtibwa Sugar bao la tatu dakika ya 73, akiunganisha krosi ya Nahodha wa zamani wa Simba SC, Henry Joseph Shindika.
  Ame Ally aliyeingia kuchukua nafasi ya Abdallah Juma aliifungia Mtibwa Sugar bao la nne dakika ya 58, kabla ya Simba SC kupata bao la pili lililofungwa na Amisi Tambwe dakika ya 89 kwa penalti, kufuatia David Luhende kumsukuma Kisiga kwenye eneo la hatari.
  Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Ivo Mapunda, William Lucian ‘Gallas’/Nassor Masoud ‘Chollo’, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Hassan Isihaka, Abdulaziz Makame, Abdallah Seseme, Said Ndemla/Pierre Kwizera dk45, Ibrahim Ajibu/Ramadhani Singano ‘Messi’ dk60, Amisi Tambwe, Awadh Juma na Twaha Ibrahim ‘Messi’/Shaaban Kisiga ‘Malone’ dk60.
  Mtibwa Sugar; Mohammed Abubakar, Hassan Mbonde/Hassan Ramadhani Kessy, David Luhende, Dickson Daudi, Ally Lundenga, Henry Joseph, Vincent Barnabas/Ally Shomary dk46, Mussa Mpakala, Abdallah Juma/Ame Ally dk58, Ibrahim Jeba na Mussa Hassan Mgosi/Mohammed Ibrahim dk58.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC ‘ROJO ROJO’, YATANDIKWA 4-2 NA MTIBWA SUGAR CHAMAZI LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top