• HABARI MPYA

  Friday, December 05, 2014

  AL AHLY YAPATA AHUENI TATIZO LA MAJERUHI, WAKALI WAWILI KUCHEZA KOMBE UWANJANI CAF KESHO CAIRO

  MKURUGENZI wa Al Ahly, Wael Gomaa, amethibitisha wachezaji wao wawili, Hossam Ghaly (pichani kulia) na Sherif Abdel Fadil wapo tayari kucheza mechi ya marudiano ya Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kesho dhidi ya Sewe Sport.
  Wote Ghaly na Fadil waliumia baada ya mchezo wa kwanza mjini Abidjan uliomalizika kwa wenyeji kushinda mabao 2-1.
  Beki wa kushoto wa Al Ahly, Sabri Rahil, alipata maumivu ya misuli katika mazoezi ya timu yake wiki hii.
  "Ghaly na Sherif Abdel Fadil walifanya mazoezi Alhamisi na wachezaji wengine na wanaonekana wapo kawaida na fiti kucheza mechi ya mwisho," amesema Gomaa.
  "Hali ya Rahil haiko wazi bado, lakini nafikiri atatusapoti kwenye mechi,".
  Timu hiyo yenye maskani yake Cairo inasumbuliwa na tatizo la majeruhi na pia itaiwakosa nyota wake Mohamed Nagi Gedo na Mahmoud Hassan 'Trezeguet,' waliopewa kadi za njano za pili katika mchezo wa kwanza.
  "Ndiyo, tutacheza mechi hii na wachezaji 15 tu wa kikosi chetu, lakini tunawaamini wote na tunajiamini. Tunaweza kufanya hivi," amesema Gomaa. Al Ahly inahitaji ushindi wa 1-0 ili kutwaa Kombe la Shirikisho kwa faida ya bao la ugenini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AL AHLY YAPATA AHUENI TATIZO LA MAJERUHI, WAKALI WAWILI KUCHEZA KOMBE UWANJANI CAF KESHO CAIRO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top