• HABARI MPYA

  Saturday, December 06, 2014

  AHLY WALE WALE WALIOITOA YANGA KWA MBINDE WABEBA NDOO YA AFRIKA

  Na Salum Esry, CAIRO
  BAO la dakika ya mwisho la Emad Meteb limeipa Al Ahly ya Misri ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa 1-0 katika fainali ya pili leo dhidi ya Sewe Sport ya Ivory Coast mjini Cairo.
  Ahly walihitaji ushindi wa 1-0 nyumbani leo baada ya kufungwa 2-1 katika mchezo wa kwanza na sasa wanainua ndoo ya CAF kwa mara ya kwanza kwa faida ya bao la ugenini, baada ya matokeo ya jumla kuwa 2-2.
  Meteb, mchezaji aliyebaki kutoka kikosi cha mafanikio cha Ahly muongo uliotangulia, alifunga bao hilo akiunganisha krosi ya Walid Soliman na kumtungua kipa Sylvain Ghobouo.
  Kikosi cha Al Ahly kilichofungwa 1-0 na Yanga SC katika mchezo wa Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo kimesherehekea ubingwa wa Kombe la Shirikisho

  Baada ya filimbi ya mwisho, Juan Carlos Garrido alijimwaga Uwanja wa Cairo kusherehekea kuwa kocha wa kwanza Mspanyola kutwaa taji la CAF.
  Kwa ujumla hilo linakuwa taji la 19 la Afrika kwa Ahly, yakiwemo nane ya Ligi ya Mabingwa, sita ya Super Cup na manne ya Kombe la Washindi.
  Ushindi wa Ahly angalau unaweza kuwa faraja kwa watu wa Misri, baada ya timu yao ya taifa kushindwa kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika.
  Ahly iliangukia kwenye Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa katika 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ambako ilianza kwa kuitoa Yanga SC ya Tanzania kwa penalti baada ya sare ya jumla ya 1-1, kila timu ikishinda 1-0.
  Na japokuwa ilionekana kama timu nyepesi wakati inaitoa Yanga kwa mbinde, lakini mwisho wa msimu Wekundu hao wanasherehekea taji la Afrika. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AHLY WALE WALE WALIOITOA YANGA KWA MBINDE WABEBA NDOO YA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top