• HABARI MPYA

  Saturday, December 06, 2014

  YAYA TOURE AWAPA RAHA MATAJIRI WA MAN CITY

  BAO pekee la Mwanasoka Bora wa Afrika, Yaya Toure limeipa Manchester City wa 1-0 dhidi ya Everton katika mchezo mkali wa Ligi Kuu ya England, usiku wa leo Uwanja wa Etihad.
  Nahodha huyo wa Ivory Coast alifunga bao hilo kwa penalti dakika ya 24 na sasa Man City wanapunguza pengo la pointi hadi kubaki tatu dhidi ya vinara wa ligi, Chelsea ambao mapema leo wamefungwa 2-1 na Newcastle.
  Mabingwa hao wa England walipata pigo dakika ya tisa tu baada ya mshambuliaji wao tegemeo Sergio Aguero kutoka nje kwa kuumia goti.
  Kikosi cha Man City kilikuwa: Hart, Zabaleta, Demichelis, Mangala, Clichy, Jesus Navas/Lampard dk78, Fernando, Toure, Milner, Nasri, Aguero/Pozo dk7, Pozo/Dzeko dk63.
  Everton: Howard, Hibbert, Jagielka, Distin, Baines, Besic/Barkley dk56, Barry, Coleman, Eto'o, Mirallas/Osman dk88 na Lukaku.
  Manchester City's Yaya Toure gives his side the lead from the penalty spot as the champions go 1-0 up 
  Yaya Toure akikimbia kushangilia baada ya kuifungia Manchester City bao pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Everton 

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2863641/Manchester-City-1-0-Everton-Yaya-Toure-scores-winner-champions-title-race.html#ixzz3L9ObnGmU 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YAYA TOURE AWAPA RAHA MATAJIRI WA MAN CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top