// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MWAMEJA, MANYIKA, PAWASA, LUNYAMILA NA MMACHINGA WAITWA KUIVAA REAL MADRID, MAKOCHA WAO MKWASA, MINZIRO NA JULIO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MWAMEJA, MANYIKA, PAWASA, LUNYAMILA NA MMACHINGA WAITWA KUIVAA REAL MADRID, MAKOCHA WAO MKWASA, MINZIRO NA JULIO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, August 15, 2014

    MWAMEJA, MANYIKA, PAWASA, LUNYAMILA NA MMACHINGA WAITWA KUIVAA REAL MADRID, MAKOCHA WAO MKWASA, MINZIRO NA JULIO

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    MAKIPA maarufu waliowahi kuwika nchini, Mwameja Mohamed na Manyika Peter wamejumuishwa katika kikosi cha Tanzania All Stars kitakachomenyana na magwiji wa Real Madrid ya Hispania, Agosti 23, mwaka huu. 
    Chini ya makocha Charles Boniface Mkwasa ‘Master’ na Wasaidizi Freddy Felix Minziro na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, Daktari Mwanandi Mkwankemwa na viongozi Mtemi Ramadhani, Hassan Mnyenye, Omar Gumbo na Hamisi Kisiwa kikosi hicho kitaingia kambini Dar es Salaam kujiandaa kwa mchezo huo wa Agosti 23, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
    Wakali wa enzi; Mohammed Hussein 'Mmachinga' kulia na Edibily Lunyamila kushoto watakumbushia enzi dhidi ya Real Madrid Agosti 23, mwaka huu Uwanja wa Taifa 

    Wengine walioItwa ni mabeki Nsajigwa Shadrack, Mecky Mexime, Boniface Pawasa, John Mwansasu, 
    Abubakar Kombo, George Masatu, Habib Kondo, 
    Viungo Suleiman Matola, Shaaban Ramadhani, Salvatory Edward, Sabri Ramadhani ‘China’, Yussuf Macho, Abdul Mashine, Abdul Maneno, Mao Mkami, Steven Nyenge, Madaraka Suleiman, Akida Makunda na Mtwa Kihwelo.
    Washambuliaji ni Monja Liseki, Iddi Moshi, Dua Said, Emmanuel Gabriel, Said Maulid, Thomas Kipese, Nasor Mwinyi ‘Bwanga’, Edibilly Lunyamila, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’, Clement Kahbuka, 
    Madaraka Suleiman na Akida Makunda. 
    Wachezaji waliotamba kuanzia La Liga, wakacheza ligi nyingine za Ulaya, Kombe la Ulaya, Ligi ya Mabingwa na Kombe la Dunia waliowahi kuchezea Real Madrid watakuja nchini Agosti 22.
    Manyika Peter atasaidiana na Mwameja Mohamed siku hiyo kuzuia michomo ya akina Luis Figo na Zidane

    Katika ziara hiyo, pamoja na kucheza mchezo wa kirafiki na kikosi maalum cha wachezaji nyota wa Tanzania Agosti 23, pia watafanya utalii katika vivutio mbalimbali, ikiwemo kupanda mlima Kilimanjaro.
    Real Madrid inakuja nchini kwa mwaliko wa kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (TSN), chini ya Mkurugenzi wake Mkuu, Farough Baghozah.
    Miongoni mwa nyota wanaotarajiwa kuja na Real nchini ni pamoja na Wanasoka Bora wa zamani wa Dunia, Mfaransa Zinadine Zidane, Mreno Luis Figo na Mbrazil, Ronaldo Lima.
    Magwiji hao wa Real tayari wamekwishafanya matangazo ya ziara yao nchini wakisema wana hamu mno ya kukanyaga ardhi ya Tanzania.
    Kampuni ya Vodacom Tanzania ni miongoni mwa makampuni yaliyojitokeza kudhamini ziara pamoja na Fastjet, Tropical, Pembe Flower, Lake Gas, EFM Radio na Ladger Plaza Bahari Beach.
    Wito umetolewa kwa makampuni zaidi kujitokeza kudhamini ziara hiyo ya kihostoria nchini.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MWAMEJA, MANYIKA, PAWASA, LUNYAMILA NA MMACHINGA WAITWA KUIVAA REAL MADRID, MAKOCHA WAO MKWASA, MINZIRO NA JULIO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top