Na Mahmoud Zubeiry, Mombasa
TIMU ya soka ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars itamkosa kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ katika mchezo wake mmoja tu, wa Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge dhidi ya wenyeji, Kenya Uwanja wa Kenyatta, Machakos Jumanne baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu katika Robo Fainali dhidi ya Uganda jana, Uwanja wa Manispaa, Mombasa.
Lakini pia, Stars iko hatarini kuwakosa wachezaji wake wawili tegemeo, Mrisho Khalfan Ngassa na Thomas Emmanuel Ulimwengu ambao ni majeruhi.
Ngassa aliumia na kutoka uwanjani dakika ya 80 jana akiwa tayari amefunga mabao mawili na kumpisha Athumani Iddi ‘Chuji’, wakati Ulimwengu alimaliza dakika 90 akiwa anachechemea kwa maumivu ya nyama.
Mshambuliaji wa Yanga SC ya Dar es Salaam, Mrisho Ngassa aliiambia BIN ZUBEIRY jana kwamba ameumia kifundo cha mguu na kuchanika mdomoni ndani na nje baada ya kuumizwa na wachezaji wa Uganda jana.
“Maumivu ni makali kote kote, yaani hapa kichwa kinaniuma,”alisema na kuongeza kuwa anasubiri kupatiwa tiba ili aone hali yake.
Kwa upande wake, mshambuliaji wa Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Ulimwengu alisema kwamba anahisi maumivu makali ya nyama.
“Kama hizi nyama zitaendelea hivi, sidhani kama nitaweza kucheza, naomba mungu nipate ahueni ili niweze kucheza,”alisema.
Stars itamenyana na wenyeji, Kenya, Harambee Stars katika Nusu Fainali ya Kwanza ya Kombe CECAFA Challenge Desemba 10, mwaka huu Uwanja wa Kenyatta, Machakos, Kenya.
Hiyo inafuatia Kenya kuifunga Rwanda 1-0 katika Robo Fainali ya pili CECAFA Challenge jioni ya jana Uwanja wa Manispaa, Mombasa Kenya, bao pekee la beki wa Azam FC ya Dar es Salaam, Joackins Atudo kwa penalti dakika ya 56.
Mapema katika Robo Fainali ya kwanza, Stars iliwatoa mabingwa watetezi, Uganda kwa penalti 3-2 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90.
Robo Fainali nyingine zitachezwa leo, Ethiopia na Sudan na Zambia na Burundi, Uwanja wa Manispaa pia.
Katika mchezo wa Tanzania na Uganda uliochezeshwa na Wish Yabarow wa Somalia, aliyesaidiwa na KInde Mussa wa Ethiopia na Mohamed Idam wa Sudan, hadi mapumziko Stars ilikuwa inaongoza kwa mabao 2-1.
Mshambuliaji wa Gor Mahia ya Kenya, Dani Sserunkuma alitangulia kuifungia Cranes bao dakika ya 16, baada ya kupokea krosi ya Hamisi Kiiza aliyemtoka Erasto Nyoni na kufumua shuti la chini lililompita kipa Ivo Mapunda.
Dakika mbili baadaye, Mrisho Ngassa aliisawazishia Stars baada ya kuwazidi ujanja na maarifa ya kisoka mabeki wa Uganda, akimalizia mpira uliopigwa na Mbwana Ally Samatta.
Mshambuliaji huyo wa TP Mazembe ya DRC, aliangushwa chini nje kidogo ya eneo la hatari na mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa akaenda kupiga mpira wa adhabu uliotinga moja kwa moja kuipatia Stars bao la pili.
Baada ya bao hilo, Stars waliendelea kuishambulia Uganda kwa kujiamini zaidi, lakini mabeki wa Cranes walisimama imara kutoruhusu mabao zaidi.
Kipindi cha pili, Stars ilipata pigo dakika ya 53 baada ya kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ kutolewa nje kwa nyekundu kwa kumchezea rafu Sserunkuma.
Uganda ikapata bao la kusawazisha dakika ya 73 kupitia kwa Martin Mpuga, aliyeunganisha kona ya Godfrey Walusimbi.
Kipa Ivo Mapunda alikuwa shujaa baada ya kuokoa penalti mbili za Dani Sserunkuma na Khalid Aucho wa Uganda na kuipa Stars ushindi wa penalti 3-2 baada ya sare ya 2-2 ndani ya dakika hizo 90.
Mbali na kuokoa penalti hizo mbili, Uganda walipoteza penalti nyingine moja baada ya Godfrey Walusimbi kupiga, wakati Hamisi Kiiza Emannuel Okwi ndiyo pekee walioifungia Cranes penalti.
Waliofunga penalti za Bara ni Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’na Erasto Nyoni, wakati Mbwana Samatta na Amri Kiemba walikosa.

![]() |
Thomas Ulimwengu aliumia nyama jana na chini Mrisho Ngassa alivyoumia jana
|

| Sure Boy atakosa mechi moja ya Nusu Fainali, mechi ya mwisho atacheza |

.png)
0 comments:
Post a Comment