BAO la dakika ya 90 la Oussama Assaidi, limezamisha Chelsea mbele ya Stoke kwa mabao 3-2 huo ukiwa ushindi wao wa kwanza katika Ligi Kuu ya England dhidi ya The Blues ndani ya miaka 38.
Winga huyo wa mkopo kutoka Liverpool, aliingia uwanjani akitokea benchi zikiwa zimesalia dakika sita na kufunga bao hilo muhimu lililmtoa kichwa chini kocha Jose Mourinho Uwanja wa Britannia.
Mabao ya Chelsea yalifungwa na Andre Schurrle dakika za tisa na 53, wakati mabao mengine ya Stoke yalifungwa Peter Crouch dakika ya 42 na Ireland dakika ya 50.
Kocha Jose Mourinho akiwa hana raha baada ya kipigo
Wachezaji wa Chelsea wakiwa hawaamini macho yao
Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo, mshambuliaji Luis Suarez ameendelea kung'ara baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 4-1 nyumbani dhidi ya West Ham.
Suarez alifunga mabao yake dakika za 81 na 84, wakati mengine yalifungwa na Demel aliyejifunga dakika ya 42 na Sakho dakika ya 47, huku la kufutia machozi la wageni likifungwa na Skrtel aliyejifunga pia dakika ya 66.
Nayo Manchester City imelazimishwa sare ya 1-1 na Southampton ugenini, Sergio Aguero akitangulia kufunga dakika ya 10 kabla ya Dani Osvaldo kuwasawazishia wenyeji dakika ya 42.
Mkali kweli: Luis Suarez (wa pili kulia) akipongezwa na wenzake
Suarez akishangilia 
Suarez akitafuta mbinu za kumtoka beki wa West Ham
Sergio Aguero akipongezwa na wenzake baada ya kuifungia bao la kuongoza Mancester City



.png)
0 comments:
Post a Comment