SIMBA imesonga mbele hatua inayofuata ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) , baada ya jana kuifunga Kiyovu ya Rwanda kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kutokana na matokeo hayo Simba imesonga mbele kwa jumla ya mabao 3-2 na sasa itakutana na ES Etif ya Algeria, ambapo mchezo wa kwanza utafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Machi 23, 24 na 25 mwaka huu na kurudiana wiki mbili baadaye jijini Algiers, Algeria.
Simba iliuanza mchezo kwa kasi, lakini washambuliaji wake Felix Sunzu, Okwi na Patrick Mafisango walishindwa kutumia nafasi kadhaa walizopata.
Kiyovu nao walijibu mapigo kwenye dakika ya 7 na 12 lakini mashuti ya washambuliaji wake Djabil Mutarambirwa na Yusuf Ndaiyishimiye yalitoka nje ya goli la Simba.
Sunzu alifunga bao la kwanza dakika ya 19 baada ya Okwi kuwalamba chenga mabeki kadhaa
wa Kiyovu na kutoa pasi nzuri kwa kiungo Mwinyi Kazimoto aliyemtengea Sunzu aliyeusukumia wavuni kiurahisi.
Simba walifunga bao la pili mfungaji akiwa Sunzu dakika ya 32 akimalizia pasi nzuri ya Okwi aliyewalamba chenga mabeki wa Kiyovu upande wa kulia kabla ya kutoa pasi kwa mfungaji.
Kiyovu walifanikiwa kupata bao mfungaji akiwa Nelly Mayanja dakika 77 aliyeingia kipindi
cha pili kuchukua nafasi ya Egide Rutayisire.
Kipa wa Simba Juma Kaseja alilazimika kufanya kazi ya ziada baada ya kuokoa mpira uliokuwa unakwenda wavuni uliopigwa na mshambuliaji Yusuf Ndaishimiye.
Dakika za mwisho za mchezo huo hali ilikuwa ngumu kwa Simba na kufanya maelfu ya mashabiki wa timu hiyo kuwa kimya kutokana na lango lao kushambuliwa mara kwa mara.
Wakati huohuo, Mwandishi Fatma Saidi anaripoti kuwa timu ya Jamhuri ya Pemba jana iliaga michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kufungwa mabao 4-1 na Hwangwe FC ya Zimbabwe mchezo uliofanyika jijini Harare, Zimbabwe.
Kwa mujibu wa viongozi wa Jamhuri ni kuwa mpaka mapumziko washindi walikuwa mbele kwa
mabao 2-0, huku bao la Jamhuri likifungwa dakika ya 80 na Suleiman Ali Nuhu.
Mchezo wa kwanza wiki mbili zilizopita Jamhuri ilifungwa mabao 3- 0 kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba.

.png)
0 comments:
Post a Comment