| Kikosi cha Simba kilichowika Afrika Jumapili, kitaendeleza cheche mbele ya Kagera kesho? |
WAKIWA
wenye furaha ya kusonga mbele kwenye Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, Simba
SC kesho watashuka dimbani, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kumenyana na Kagera
Sugar ya Bukoba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Simba
iliitupa nje Kiyovu Sport ya Rwanda Jumapili kwa ushindi wa mabao 2-1 unaofanya
jumla ya mabao 3-2, baada ya sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza wiki mbili
zilizotangulia mjini Kigali.
Sasa,
Wekundu hao wa Msimbazi wanahamishia hasira zao katika Ligi Kuu, ambayo kama
ilivyo England, Manchester United na Manchster City zinakabana koo ile mbaya kuwania
taji, nao wanakwidana kisawasawa na wapinzani wao jadi, Yanga katika vita ya
mwali.
Simba
ina pointi 37 sawa na mabingwa watetezi, Yanga lakini wao wako juu kwa sababu
ya baop moja wanalowazidi wababe wao hao katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa
Ligi Kuu.
Kocha
wea Simba, Mserbia Milovan Curkovick hatarajiwi kufanya mabadiliko makubwa
katika kikosi chake hasa ikizingatiwa Jumamosi alishinda mechi ya michuano ya
Afrika.
Juma
Kaseja, kama kawaida anatarajiwa kulinda lango, akisaidiwa na mabeki Nassor
Masoud ‘Chollo’ kulia, Amir Maftah kushoto na katikati Kelvin Yondan na Juma Nyosso
waliosaidiwa na Patrick Mafisango katika kiungo cha ulinzi.
Mwinyi
Kazimoto anasumbuliwa na nyama za paja na yuko shakani kucheza leo, lakini
Shomary Kapombe au Jonas Mkude mmoja wao anaweza kuziba pengo lake.
Uhuru
Suleiman anaweza kuanza kulia mbele na kushoto Salum Machaku wakati Mzambia
Felix Mumba Sunzu Jr aliyetupia mawili yote nyavuni katika ushindi wa 2-1 dhidi
ya Kiyovu Jumamosi atakuwa na Mganda Emanuel Okwi katika safu ya ushambuliaji.
Sunzu
na Okwi walicheza kwa ushirikiano mzuri Jumamosi ambao bila shaka Milovan atapenda
uendelee.
Hata
hivyo, Nahodha Haruna Moshi ‘Boban’ ataikosa mechi ya leo, kwa sababu bado
anatumikia adhabu kwenye Ligi Kuu.
Kagera
Sugar hawatarajiwi kuwa wanyonge kwa Simba leo, kwani kihisto4ria timu hii
kutoka mashamba ya miwa ya Misenyi imekuwa ikimtoa sana nishai Mnyama.
Mwaka
2005, Kagera Sugar iliifunga Simba 2-1 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na kutwaa
Kombe la Tusker, enzi hizo kikosi chake kikiundwa na wakali kama Mrisho Ngassa,
Omary Changa, Yussuf Macho, Vincent Barnabas, Shamte Ally, Shijja Mkinna na
Paul Kabange.
Ukiwauliza
Simba ilikuwaje wakakosa ubingwa msimu uliopita, katika moja ya sababu
wataitaja na Kagera pia- hivyo hii ni timu yenye historia ya kuwanyima raha
wana Msimbazi na hii inamaanisha gemu la leo litakuwa tamu.
Kocha Msaidizi wa Kagera Sugar, Mrage Kabange, amesema
anawahofia sana Okwi na Sunzu katika mchezo wa leo, hasa baada ya kucheza soka
adimu Jumapili na kutoa mchango mkubwa Simba ikiitoa Kiyovu.
“Soka siyo siasa, ukweli ni kwamba Okwi na Sunzu wana
viwango vya juu, hivyo nimepanga kikosi changu cha kuwadhibiti, ili
wasilisogelee lango letu,” alisema. Kagera Sugar inashika nafasi ya nane,
kutokana na pointi zake 24.
Mara
ya mwisho timu hizo zilipokutana Septemba 18, mwaka jana zilifungana bao 1-1,
Uwanja wa Taifa. Mambo yatakuwajen Taifa leo? Twendeni tukaone.
REKODI YA SIMBA NA KAGERA:
Septemba 18, 2011
Kagera Sugar
1-1 Simba
Machi 29, 2011
Simba 0-0
Kagera Sugar
Oktoba 27, 2010
Kagera Sugar
0-2 Simba
Februari 3, 2010
Kagera Sugar
1-1 Simba
Septemba 10, 2009
Simba 2-0
Kagera Sugar
Aprili 5, 2009
Kagera Sugar
0-2 Simba
Oktoba 14, 2008
Simba 1-0
Kagera Sugar
Aprili 19, 2008
Kagera Sugar
0-1 Simba
Oktoba 13, 2007
Simba 2-1
Kagera Sugar
Oktoba 18, 2006
Simba 2-1
Kagera Sugar
Juni 3, 2006
Kagera Sugar
1-0 Simba
(Kagera wakapewa ushindi wa mezani
2-0, kwa Simba kumchezesha Mussa
Mgosi akiwa ana kadi tatu za njano)
Septemba 28, 2005
Kagera Sugar
0-2 Simba
Mei 25, 2005
Simba 0-1
Kagera Sugar


.png)
0 comments:
Post a Comment