• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 10, 2009

  UPINZANI WAMTISHA HENRY JOSEPH SIMBA

  Henry Joseph, hapa alikuwa Norway alipokwenda kufanya majaribio


  KIUNGO wa Simba, Henry Joseph ‘Shindika’, amesema klabu yake imetengemaa kutokana na upinzani uliopo ndani ya kikosi chao.
  Joseph amerejea Jumatano iliyopita, akitoke nchini Ivory Coast, alipokwenda kushiriki Kombe la Mataifa Afrika, kwa wachezaji wa ndani CHAN na timu ya taifa, Taifa Stars.
  Akizungumza jijini Dar es Salaam, Joseph alisema wachezaji wote waliokuwa huko, wamekuta ushindani na kukifanya kikosi chao kiwe na uwezo mkubwa.
  Alisema siyo jambo la ajabu endapo baadhi ya wachezaji wa Stars, wakaanzia benchi kutokana na uimara wa wachezaji hao waliobaki na Simba, wakati wao walipokwenda Ivory Coast.
  “Sasa Simba imetengemaa, wachezaji wote wanacheza mpira kwa kasi na ushindani mkubwa kitu kitakachotusaidia,” alisema.
  “Naamini tutafika mbali zaidi, ingawa ubingwa tunaweza kukosa, lakini siyo nafasi ya pili inayoliliwa pia na timu zaidi ya tatu,”
  Klabu hiyo inayonolewa na Mzambia, Patrick Phiri, ipo kwenye nafasi ya tatu, huku mtani wake Yanga SC, ikiwa kileleni mwa ligi hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: UPINZANI WAMTISHA HENRY JOSEPH SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top