• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 12, 2009

  YANGA, WHITECAPS YAINGIZA MILIONI 23 TU!

  Tegete aliyefunga mabao mawili, wakati Whitecaps inalala 3-0 kwa Yanga


  MECHI ya kirafiki kati ya Yanga na Vancouver Whitecaps ya Canada iliyochezwa Jumatatu wiki hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, imeingiza jumla ya Shilingi 23,148,000 kutokana na mashabiki 4,490 waliokata tiketi.
  Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Frederick Mwakalebela alisema leo mchana kwamba, mapato hayo yametokana na viingilio vya aina tano vilivyopangwa.
  Alisema VIP A, jumla ya mashabiki 76 waliingia huku tiketi zake zikiuzwa kwa 20,000, VIP B waliingia watu 186, wakati VIP C waliingia mashabiki 236.
  Katibu huyo alisema katika viti vya rangi ya chungwa waliingia mashabiki 769, jukwaa la mzunguuko waliingia mashabiki 4226 hivyo jumla ya mashabiki wote walioshuhudia mchezo huo kuwa ni 4490.
  Leo Whitecaps iliyopigwa 3-0 na Yanga inamenyana na Simba Uwanja wa Uhuru, zamani Taifa mjini Dar es Salaam.
  Wakati huo huo: Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara, inatarajiwa kuendelea kesho kwa kuzikutanisha Villa Squad na JKT Ruvu ya Pwani, Uwanja wa Uhuru, zamani Taifa mjini Dar es Salaam.
  Mchezo huo unatarajiwa kuwa wa kusisimua kutokana na kuzikutanisha timu ambazo zenye mitazamo tofauti, JKT ikiwania nafasi ya pili na Villa ikipigana kuepuka balaa la kushuka daraja, hivyo kila mmoja itahitaji kwa udi na uvumba kushinda.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA, WHITECAPS YAINGIZA MILIONI 23 TU! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top