• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 09, 2009

  MAMA WA BURUNDI APEWA TUZO NA IOC


  RAIS wa Shirikisho la Soka Burundi (FFB), Lydia Nsekera (pichani kulia), amepewa tuzo ya heshima na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) Alhamisi wiki iliyopita kutokana na kuwa mwanamke aliye mstari wa mbele kwenye kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya soka
  IOC ilimkabidhi tuzo hiyo, iitwayo Wanawake na Michezo, Nsekera na viongozi wengine katika sherehe zilizofanyika jengo la makumbusho la Olimpiki mjini Lausanne, Uswisi.
  Mwaka 2004 Nsekera alikuwa mwanamke wa pili Afrika kuongoza shirikisho la soka la nchi, baada ya Sombo Izetta Wesley wa Liberia.
  Chini ya Nsekera, timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Burundi imetwaa ubingwa wa CECAFA na pia nchi hiyo iliandaa michuano ya kwanza ya soka ya wanawake.
  Washindi wengine wa tuzo za IOC walikuwa ni Maria Caridad Colon Ruenes wa Cuba, Arvin Dashjamts wa Mongolia, Danira Nakic Bilic wa Croatia na Auvita Rapilla wa Papua New Guinea
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAMA WA BURUNDI APEWA TUZO NA IOC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top