• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 28, 2009

  KIFUKWE, MALINZI WALIFANYA KAZI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU YANGA

  ALIYEKUWA rais wa Yanga, Francis Kifukwe na Katibu Mkuu wake, Jamal Malinzi enzi za uongozi wao kwenye klabu hiyo. Jamaa hawa waliiongoza klabu katika wakati mgumu mno, ikiwa haina mfadhili, lakini bado waliweza kuifanya itwae mataji na kufurukuta kwenye michuano ya Afrika.
  Mwaka 2007, wakati huo tayari Malinzi amekwishajiuzulu Kifukwe aliiwezesha Yanga kufika raundi ya Pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kutolewa na Esperance ya Tunisia.
  Kwa kutolewa huko, Yanga ilifanikiwa kuangukia kwenye mechi za mchujo kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho, ambako huko nako ilitolewa na El Merreikh ya Sudan.
  Hivi sasa, Yanga ikiwa ina wafadhili wawaili, Kilimanjaro Beer na Yussuf Manji, aliyesajili kikosi kikali zaidi, lakini mafanikio yake hayaendani na hali halisi.
  Yanga si ya kujivunia ubingwa wa Bara ikiwa na kikosi cha nyota kama iliyonao, ambao inasemekana usajili wake uligharimu si chini ya Milioni 500. bongostaz inawapongeza akina Kifukwe kwa kazi nzito waliyofanya zama zao na kuwapasha viongozi wa sasa chini ya Mwenyekiti, Imani Madega wahakikishe timu inafanya vizuri na klabu inakuwa na hali nzuri pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KIFUKWE, MALINZI WALIFANYA KAZI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top