• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 14, 2009

  MAN UNITED YATOTA 4-1 KWA LIVERPOOL

  Torres akiwapungia mkono mashabiki baada ya kufunga bao
  Mwamuzi akimpa kadi nyekundu Vidic baada ya kumchezea rafu Gerrard

  Gerrard akishangilia bao lake


  MANCHESTER, England
  Manchester United jana iliangukia pua katika uwanjani wake wa nyumbani baada ya kulala kwa mabao 4-1 mbele ya Liverpool.
  Katika mechi hiyo, Man United ndiyo iliyokuwa ya kwanza kuandika bao katika dakika ya 21 lililofungwa kwa penalti na Cristiano Ronaldo.
  Man United ilipata penalti hiyo baada ya kipa wa Liverpool, Jose Reina kumdaka mguu Ji Sung Park wa Manchester United.
  Reina alilazimika kumdaka mguu Park baada ya mchezaji huyo kuinasa pasi ya Carlos Tevez na kuizidi kasi safu ya ulinzi ya Man United.
  Liverpool ilisawazisha bao hilo katika dakika ya 27 baada ya Fernando Torres kumzidi kasi na nguvu beki mahiri wa Man United Nemanja Vidic na kumchambua kipa wa Man United Edwin Van Der Sir.
  Bao hilo lilitokana na mpira wa mbali uliopigwa na Martin Skrtel kutoka lango la Liverpool na ndipo Torres alipounyangÕanya mpira kutoka kwa Vidic na kufunga bao hilo.
  Katika dakika ya 43 Liverpool iliandika bao la pili lililofungwa kwa njia ya penalti na Steven Gerrard.
  Liverpool ilipata penalti hiyo baada ya Patrice Evra kumuangusha Gerrard eneo la hatari wakati kiungo huyo akikaribia kuonana na kipa, Van der Sir.
  Bao la tatu la Liverpool lilipatikana katka dakika ya 75 ya mchezo huo mfungaji akiwa ni Fabio Aurelio kwa mpira wa adhabu uliojaa wavuni.
  Adhabu hiyo ilitokana na rafu aliyochezewa Gerrad na Vidic na ndipo mwamuzi alipoamuru upigwa mpira wa adhabu ambao Aurelio aliutumia vyema.
  Bao la nne la Liverpool lilijazwa kimiani na Andrea Dossena katika dakika ya 90, Dossena alifunga bao hilo baada ya kuunganisha moja kwa moja mpira uliopigwa na Reina.
  Baada ya kuinasa pasi hiyo, Dossena alimchungulia kipa wa Man United na kupiga mpira wa juu kiufundi ambao ulimshinda Van Der Sar ambaye alishatoka golini na hivyo kubaki akiuangalia unavyokwenda wavuni taratiiibu. Matokeo hayo yanazidi kuibua matumaini mazuri ya Liverpool kushika usukani kwani hadi sasa timu hiyo ina pointi 61 tofauti ya pointi nne na Man United inayoshika usukani. Hata hivyo, United ina mchezo mechi moja mkononi.
  Kwa ushindi huo, Liverpool inakuwa imekamilisha msimu wa Ligi Kuu ya England ikiwa vinara mbele ya United baada ya kuilaza mabao 2-1 katika mechi ya mzunguko wa kwanza iliyochezwa Septemba mwaka jana.
  Mabao ya Liverpool yalifungwa na Ryan Babel na Wes Brown aliyejifunga wakati bao pekee la Man United lilifungwa na Tevez.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN UNITED YATOTA 4-1 KWA LIVERPOOL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top