• HABARI MPYA

  Thursday, March 19, 2009

  TUZO ZA KILIMANJARO 2009

  Makamu Mwenyekiti wa Tuzo za Kili, John Dilinga akizungumzia tuzo za mwaka huu  KAMPUNI ya bia nchini (TBL) kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro Premium Lager, leo tarehe 18 Machi 2009, imetangaza rasmi majina ya wasanii na wanamuziki waliopendekezwa ili waanze kupigiwa kura kuwania tuzo za muziku za Tanzania 2009, maarufu kama KILI Music Awards 2009.
  Akiongea na waadishi wa habari wakati wa kutangaza majina hayo jijini Dar es Salaam, Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Oscar Shelukindo alisema "TBL kupitia kinywaji chake mkipendacho cha Kilimanjaro Premium Lager inayo furaha kubwa kuweka hadharani leo majina ya wasanii, watayarishaji wa muziki na wanamuziki wenyewe ili Watanzania kote nchini waanza mchakato wa kuwapigia kura ili tupate washindi bora kabisa wa 2009 Katika KILI Music Awards kama tulivyokwisha fanya katika mashindano haya kwa miaka kadha iliyopita" Alisema Oscar Shelukindo.
  Meneja huyo wa bia ya Kilimanjaro aliongeza kuwa wanachotakiwa kufanya Watanzania ni kuwachagua wanamuziki na wasanii wanaowavutia watakaokuwa katika makundi 20 kwa kuwapigia kura kupitia namna kadha ikiwa ni pamoja na njia ya ujumbe mfupi wa maneno (SMS), kuponi za magazeti, kupitia tuvuti www.kilitimetz.com na kwa njia ya barua pepe kwenda vote@kilitimetz.com
  "Ikumbukwe kuwa dhumuni kuu la Tuzo za Kili Music Awards ni lile lile siku zote ambalo ni kukuza sanaa ya muziki nchini, kuvumbua vipaji vipya kupitia mashindano ya Kanda, kutambua mchango wa wanamuziki wakongwe pamoja na kuwahamasisha Watanzania kupenda na kudhamini muziki na mchango wa wanamuziki wa Kitanzania katika kukuza sanaa hii hapa nchini kwetu na kuhakikisha kuwa muziki wa nje haupati umaarufu kushinda wetu" aliongeza Oscar Shelukindo.
  Sherehe za kuwatunza wanamuziki washindi wa Tuzo za 2009 KILI Music Awards zitafanyika mapema mwezi wa Aprili 2009, ambapo baada ya hapo kutakuwa na ziara maalum ya washindi wa Tuzo za Kili Music Awards na kutumbuiza katika majukaa ya miji mbalimbali hapa nchini.

  WAKALI WA TUZO ZA KILI 2009

  Maandalizi ya Tuzo za Muziki za Kili..zinazotarajiwa kufanyika Jumamosi hii kwenye Hoteli ya Kempinski yamekwishakamilika.Kwa mujibu wa waandaaji wa tuzo hizo,kwa mwaka huu zitaonyeshwa moja kwa moja kupitia vituo vya televisheni ili watu mbalimbali waweze kushuhudia.Katika tuzo hizo, washindi watatangazwa na kuzawadiwa tuzo zao na washiriki wengine kila mmoja watapata cheti.Katika hatua nyingine,hakutakuwa na tiketi za kuuza kama iliyozoeleka miaka yote ila kutakuwa na mialiko ambayo wadhamini..ambao ni kampuni ya bia Tanzania (TBL) watatoa kwa watu maalumu tu.Watanzania wametakiwa kuwapigia kura wasanii wanaowapenda katika kipindi hiki cha mwisho upigaji kura huo unaweza kufanywa kupitia tovuti, barua pepe, ujumbe mfupi na kuponi zilizopo kwenye magazeti mbalimbali.Katika tamasha hilo, bendi ya muziki ya FM Academia imepangwa kupamba jukwaa pamoja na Dar Modern Taarab, wasanii Chidi Benz, TID, Mwasiti na kundi la THT. Kutoka Uganda ni Ngoni na Kenya ni Redson.
  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo za Muziki Tanzania, John Dilinga akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu wasanii walioingia katika kuwania tuzo za muziki za Kilimanjaro 2008, wakati wa mkutano uliofanyika jijini Dsm hivi karibuni. PICHA/JOHN BADI.
  Albamu bora ya taarabu inawaniwa na Gharika la Moyo (Dar Modern Taarab), Kazi ya Mungu haiingiliwi (Jahazi), Raha ya Mapenzi (Zanzibar Stars), Tupendane wabaya waulizane (Jahazi) na Vishanshuda (Dar Modern). Nyimbo bora za miondoko hiyo ni Pembe la Ng'ombe (Dar Modern), Kazi ya Mungu haiingiliwi (Jahazi), Raha ya mapenzi (Zanzibar Stars), Tupendane wabaya waulizane (Jahazi) na Vishanshuda (Dar Modern).
  Katika wimbo bora wa mwaka zipo Bembeleza (Marlaw), Cinderera (Kiba) Mtaa wa kwanza (Twanga), Pembe la Ng'ombe (Dar Modern) na Siku hazigandi (Lady Jay Dee).
  Wimbo bora wa bendi ni Kilio cha Mpemba (Double M), Kuachwa ( Khalid Chokoraa), Maneno maneno (Bambino), Mtaa wa Kwanza (Twanga) na nguvu za giza (Twanga).
  Albamu bora ya bendi ni Kwangu ni wapi (Hussein Jumbe), Mtaa wa kwanza (Twanga) na wimbo bora wa R & B unawaniwa na Bembeleza, Binti Kiziwi, Cinderera, Haiwezekani na wachuja.
  Wimbo bora wa asili unawaniwa na Alongole Siza Mazongela (Wazazi Cultural Troupe), Itumba Mbwewe (Kalunde Band), Mama Dory Lima (Richard Mziray), Mauaji ya maalbino (Malima Mjinja na Maringo Band), Ngoma zetu (Chemundu Gwao).
  Albamu bora ya asili ni Enyanyinyi nyota (Kakau Band), Kisiwa cha Ukerewe (Malima na Maringo Band), Magoma moto (Che Mundu Gwao) na Waafrika wa Wanne Star.
  Wimbo bora wa Hip hop unawaniwa na Hapo sawa (Profesa Jay), Kazi ipo (TMK Wanaume Family), Ndege tunduni (TMK Wanaume Halisi), Ni hayo tu (Fid Q) na Umenisoma wa Chidi Benz wakati wimbo bora wa Reggae na Ragga unawaniwa na Baby Candy (Dully Sykes), Buzi ( PJ Mhina), Kati yetu (Besta Prosper Rugeiyamu), Nolilaga na One Day (Jumanne Iddi)
  Msanii bora wa Rap itawaniwa na Chidi Benz, Fid Q, Langa, Mwana FA na Profesa Jay huku wimbo bora wa Afrika Mashariki ukiwakutanisha Banjuka (DNA Kenya) Jangu (Obsession, Uganda), Kwa heri (Jua Kali, Kenya), Mising my baby (Amani, Kenya) na Yoyo (Michael Rose (Uganda).
  Mtunzi bora wa muziki utawaniwa na Banzastone, Deo Mwanambilimbi, Judith Wambura, Mzee Yussuf na Said Comorien huku Mtayarishajji bora ikiwakutanisha Allan Mapigo, Lamar, Makochali, Roy Bukuku na Said Comorien wakati mwandikaji bora wa nyimbo ikiwa ni mpambano kati ya Chid Benz, Deo Mwanambilimbi, Jay Dee, FA na Profesa Jay.
  Mtayarishaji bora wa video wapo Chapakazi, Emptysoul, Visual Labs, Wananchi Video na Jupiter Production.
  Wimbo bora wa mwaka wa Zouk unawaniwa na Mac Muga wa Ali Kiba, Mbali nami (Bushoke), Nimekosa (Voice Wonder) Nyota yako (TID) na Tanita wa Q Chillah wakati wimbo bora wa kushirikiana utazikutanisha Habari ndiyo hiyo (AY, FA), Ni hayo tu (Fid Q, Profesa Jay na Langa), Tell Me why (Makamua, Chid Benz), Unga robo (TMK Wanaume Halisi, Fid Q na Prof Jay) na Najua nakupenda uliowashirikisha Queen Darleen na Ali Kiba.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TUZO ZA KILIMANJARO 2009 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top