• HABARI MPYA

    Tuesday, March 10, 2009

    YANGA HAOOO, WAIFUATA AL AHLY

    MABINGWA wa Tanzania, Yanga (pichani) jioni hii wanaondoka mjini Dar es Salaam kwenda Cairo, Misri wakiwa na kikosi cha wachezaji 20 na viongozi 10 tayari kwa mchezo dhidi ya wenyeji Al Ahly, katika Uwanja wa International mjini humo Jumapili.
    Pambano hilo linatarajiwa kufanyika saa moja usiku wa Jumapili jijini Cairo na wakati Yanga inaondoka leo, itawasili Misri saa nne na robo usiku wa leo.
    Akizungumza na Waandishi wa Habari jana, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Iman Madega, alisema kwamba maandalizi watondoka leo saa 9:00 kwa Ndege ya Shirika la Kenya (KQ).
    Katika msafara huo utakaoongozwa na Madega, kikosi cha Yanga kitakuwa na makipa wake wawili tegemeo, Juma Kasseja na Mserbia Obren Curkovic.
    Wachezaji wengine ni Abdi Kassim, Vincent Barnabas, Mike Barasa, Amir Maftaha, Athuman Iddy ‘Chuji’, Jerry Tegete, George Owino, Halfan Ngasa, Nadir Harob “ Canavaro” na Ben Mwalala.
    Wengine ni Kiggy Makassy, Geofrey Bonny, Nurdin Bakar, Shedrack Nsajigwa, Wisdom Ndlovu, Fred Mbuna, Boniface Ambani na Shamte Ally.
    Benchi la ufundi litaongozwa na Kocha Mkuu, Dusan Kondic, kocha msaidizi Spaso Sokolovisc na kocha wa timu ya Vijana, Livujnon Ordan.
    Wengine ni kiongozi kutoka TFF, Alex Mgongololwa, Katibu Mkuu Lucas Kisasa, Katibu wa Kamati ya Mashindano, Emanuel Mpangala, Meneja wa timu, Ken Mkapa, mchua misuli Nassor Matuza na daktari wa timu, Jackob Nyange.
    Madega alisema kuwa wanakwenda kwenye mashindano si kushiriki, wakiwa wana imani kwamba watafanya vizuri.
    Yanga imekuwa ikifanya mazoezi saa 12 jioni kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo na itarejea jijini Dar es Salaam Machi 17.
    Mchezo wa marudiano unatarajiwa kufanyika baada ya wiki mbili jijini Dar es Salaam. Yanga inatakiwa kushinda pambano hilo kwa idadi kubwa ya mabao, ili iweze kujiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA HAOOO, WAIFUATA AL AHLY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top