• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 14, 2009

  STARS YALAZIMISHWA SARE NA VANCOUVER


  TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, leo imetoka sare ya bila kufungana na Vancouver Whitecaps ya Canada, katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Stars katika mechi hiyo ilionyesha uhai, lakini tatizo kubwa ilikuwa ni katika safu ya ushambuliaji, iliyoshindwa kuziona nyavu.
  Shambulizi la nguvu la Stars lilifanywa katika dakika ya 34, baada ya Nizar Khalfan kugongeana pasi safi na Zahor Pazi, lakini mabeki wa Vancouver walikuwa imara kukabiliana na shambulizi hilo.
  Dakika ya 42 Stars ilikosa bao, baada ya Pazi kushindwa kuitumia vizuri kazi iliyofanywa na Mwinyi Kazimoto, aliyemuunganishia pasi safi.
  Hata pamoja na kukosa bao hilo,
  Pazi na Kazimoto leo walionekana kuwa kivutio mbele ya mashabiki na watazamaji waliohudhuria mechi hiyo.
  Dakika ya 50 tena Stars waligongeana vizuri, lakini tatizo likawa umaliziaji ambako shuti la Nizar lilitoka nje ya lango.
  Baada ya kosakosa hizo, kocha wa Taifa Stars, Marcio Maximo (pichani juu) aliendelea na mabadiliko ya hapa na pale kwa kumtoa Nizar na kumuingiza ndugu yake, Razak Khalfan.
  Stars: Shaaban Dihile, Aziz Nyoni, Juma Jabu, Kelvin Yondani, Salum Sued, Shaaban Nditi, Zahor Pazi/Uhuru Suleiman, Henry Joseph/Jabir Aziz, Mussa Hassan Mgosi/John Bocco, Nizar Khalfan/Razak Khalfan na Mwinyi Kazimoto.
  Vancouver: Nolly, Luca Bellisomo, Wesley Charles, Justin Thompson, Takashi Hirano, Gordon Chin, Mason Trafford, Martin Nash, Vicente Arze/Tyreil Burgess, Charles Gbeke/Gaden Sisanoh na Marlon James.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: STARS YALAZIMISHWA SARE NA VANCOUVER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top