• HABARI MPYA

  Monday, March 16, 2009

  AMBANI ALIA NA REFA CAIRO


  BONIPHACE Ambani amesema kwamba mwamuzi wa mchezom baina ya Yanga na Al Ahly alikuwa akiwapendelea wenyeji, ndio maana walifungwa 3-0 juzi mjini Cairo.
  Akizungumza na bongostaz kutoka Cairo, Ambani alisema kwamba mwamuzi huyo alifanya kila aliloweza kuhakikisha Yanga haipati bao siku hiyo, ikiwemo kwanyima penalti ya halali.
  "Nilipiga mpira kuelekea langoni, ulikuwa umekwishampita kipa, lakini wao mmoja akauzuia kwa mkono, ila refa hakutoa penalti,"alisema Ambani.
  Hata hivyo, mshambuliaji huyo alisema kwamba nao wanarudi nyumbani kujiandaa na mchezo wa marudiano, wakiwa na dhamira kubwa ya kulipa kisasi.
  "Kama wametufunga kwao 3-0, kwa nini sisi tusiwafunge 4-0 kwetu, sisi tuna uwezo, tutalipa kisasi,"alisema Ambani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AMBANI ALIA NA REFA CAIRO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top