• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 14, 2009

  NAKAAYA ANAYEWASHIKA MPAKA BASI...

  Nakaaya akiwa na Ray na ndugu yake Tamara
  Nakaaya akiwa na Tina Koroso aliyeshirikii naye Tusker Project Fame

  Nakaaya
  HUWEZI kuzungumzia wanamuziki wa kike wanaofanya vizuri kwenye anga ya muziki wa Tanzania hivi sasa, bila kulihusisha na jina la mwanadada Nakaaya Sumari.
  Kimwana huyo ambaye ni dada wa Miss Tanzania 2005, Nancy Sumary kwa sauti yake tamu inayosikika vizuri zaidi kwenye kibao Mr Politician, amejizolea mashabiki kibao.
  Nakaaya Sumari alizaliwa mkoani Arusha, nchini Tanzania mwaka 1982. Tukimalizia hapa inaweza kuwa habari kweli jamani? Hatutakuwa tumekosea hivi... Ngoja tuendelee.. Nakaaya ni dada wa kwanza katika familia yenye watoto watano, umeona bwana? Na moja kati ya wadogo zake ni Nancy Sumari, ambaye ni Miss Tanzania wa mwaka 2005 ambaye pia alifanikiwa kunyakua taji la Miss World Africa mwaka huo huo. Wengi mlianza kumjua baada ya cheche alizozitoa kwenye shindano la uimbaji linalojulikana kwa jina la Tusker Project Fame, ambalo liliruka hewabi kuanzia tarehe 10 Oktoba, mpaka Desemba 17, ilikuwa ni mwaka 2006 na lilikuwa ni shindano kwa vijana kwa Afrika ya Mashariki. Yawezekana mafunzo aliyoyapata akiwa huko ndio yakasababisha akomae zaidi kimuziki, maana wakiwa kambini wakati wa mashindano, walikuwa wakipewa mbinu hizi na zile, yote haya yalikuwa ni katika kuhakikisha kwamba, ...wanakuwa wanamuziki wa kweli.. Na huu ni kama ukweli hivi, maana baada ya kurudi huko ndio tukaanza kuona cheche, swali la kujiuliza ni kwamba, mwanzoni alikuwa wapi? Haya ni kama matunda ya Tusker Project Fame hivi... Mwaka 2007 alitulia, lakini mwaka uliofuata, yaani 2008, mwezi wa pili tu akaangusha albam, ..Nervous Conditions ambayo ilianguka sambamba na ngoma yake ya kwanza, iliyokwenda kwa jina la Malaika ila watu kama hawakuelewa hivi... Basi akaachia ngoma ingine, ambayo ilikwenda kwa jina la Mr Politician, mtayarishaji akiwa Ambroce Dyga wa Mandugu Digital, na video ikafanywa na Visual Lab. Afrka mashariki nzima ikamuelewa, na kitu kikubwa ambacho kilimuweka juu, binti alienda Marekani akatengeneza CD zake akauza mkononi, na huko alifanya matamasha mawili matatu, ...umemuelewa? Kikubwa kimetokea mwaka huu bwana, wakati binti alipohudhuria semina ya kisanii, baada ya Taasisi wa KiDanish inayojulikana kwa jina la anish Centre for Culture and Development (DCCD), hukooo Copenhagen. Akashiriki kwenye semina iliyokuwa ikijadili muziki na nafasi yake katika nchi za dunia ya tatu. Baada ya semina, binti akaangusha Gig moja ambalo alifanya onesho kali ndani ya ukumbi wa Copenhagen Jazz House, kesho yake, ..akafanya kipindi na kituo kimoja cha huko kinachoutwa DR2 kipindi cha ?Deadline?. Hapo ndipo Sony Music Entertainment alipomuona, na hivi tunavyoongea, ..wameshamnyakua na kusaini naye mikataba, na binti anakula hizi Bata mbili tatu, maana yuko lebo moja na watu kama akina Mariah Carey umeona bwana na wanamuziki wengi maarufu. Peter Gr? wa Sony Music Entertainment amesema hawajutii mpaka sasa, wamepata kipaji ambacho kinaiwakilisha vema sana Afrika ya Mashariki. Huyu ni mwanamuziki wa kwanza wa Tanzania kupata deal la kimataifa, sisi tunamuita nakaaya The International!

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NAKAAYA ANAYEWASHIKA MPAKA BASI... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top