• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 16, 2009

  SMITH AENDELEZA UBABE KWA WATANZANIA, AMPIGA NA MATUMLA

  Vibonde wa Smith, Cheka na Matumla aliyesimama kwenye mzani. hapa walikuwa wakipima uzito kabla ya pambano lao mjini Morogoro.


  BONDIA Paul Smith juzi aliendeleza ubabe wake kwa mabondia wa Tanzania, baada ya kumpiga Rashid Matumla na kutwaa taji la WBA International, uzito wa Super Middle.
  Katika pambano hilo lililofanyika ukumbi wa MEN Arena, Manchester, Uingereza Matumla alisalimu amri kwa kipigo cha Technical Knockout (TKO) raundi ya pili.
  Hili linakuwa pambano la pili mfululizo kwa Matumla kupigwa, kwani mwezi uliopita mbabe huyo alipigwa kwa pointi na Francis Cheka mjini Morogoro. Smith pia aliwahi kumpiga Cheka kwa pointi mwaka jana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SMITH AENDELEZA UBABE KWA WATANZANIA, AMPIGA NA MATUMLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top