• HABARI MPYA

  Friday, March 20, 2009

  YANGA YAPUNGUZWA KASI NA TFF

  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeipokonya Yanga pointi mbili, ambazo iliwapa mezani baada ya mchezo dhidi ya Polisi Morogoro mjini humo.
  Timu hizo zilitoka sare, lakini kutokana na Maafande hao wa Morogoro kudaiwa kutumia mchezaji aliyekuwa anatumikia adhabu ya kadi, Kamati ya Mashindano iliamua kuipa ushindi Yanga.
  Hata hivyo, Polisi ilikata rufani kupinga uamuzi huo na wakafanikiwa kushinda, hivyo Yanga kupokonywa pointi mbili na Maafande kurejeshewa pointi yao moja waliyoichuma kwa jasho.
  Ligi Kuu ya Bara inatarajiwa kuendelea baadaye jioni leo, wakati Yanga itakapokuwa ikimenyana na Toto Afrika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
  Yanga ikishinda mchezo huo, itafikisha pointi 46, ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ya Ligi Kuu, hivyo kujitangazia ubingwa wa Tanzania Bara kwa mara ya 22. mchezo mwingine leo ni kati ya Kagera Sugar dhidi ya Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Kagera ambayo ni timu pekee yenye uwezo wa kufikisha pointi 45 ikishinda mechi zote kuanzia leo kwa sasa ipo katika nafasi nzuri ya kuupata Uwakilishi wa nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika mwakani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAPUNGUZWA KASI NA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top