• HABARI MPYA

  Tuesday, March 10, 2009

  KASEJA: CHONGENI, LAKINI TUTAISHIKISHA ADABU AL AHLY

  Kaseja aliyemrukia Athumani Iddi 'Chuji' katika moja ya mechi za Yanga


  KIPA tegemeo Yanga, Juma Kaseja amesema kwamba pamoja na watu wengi kuidharau timu yao kwamba itaambulia kapu la magoli mbele ye Al Ahly Jumapili hii katika mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza, Ligi ya Mabingwa Afrika mjini Cairo, lakini yeye anaamini watafanya vizuri.
  Akizungumza na DIMBA mjini Dar es Salaam juzi, Kaseja alisema yeye amekuwa mzoefu na mechi kama hizo hasa wachezaji wa ukanda huo wa Misri, lakini pamoja na hivyo amesema watafanya kazi kubwa ili waweze kurudi na ushindi kwa kujitengenezea nafasi nzuri ya kusonga mbele.
  “Kama Yanga tupo vyema kila kitu tunakipata tutaenda Cairo kupigana kufa na kupona mchezo utakuwa mgumu, mimi nasema hivi kwa sababu hawa waarabu bwana kwangu sio wageni sana, maana nilipokuwa Simba nimecheza nao sana na wana fitina sana, lakini sisi tutaenda kwa lengo la kwenda kushinda na kufanya vizuri ili hapa nyumbani tutakaporudiana tuweze kulinda heshima yetu ”alisema.
  Aliongeza kwamba wachezaji wote wanatakiwa kutulia wasifuate maneno ya mitaani kwani Al Ahly inaweza kuwatisha kwa jina kubwa ambalo halina kitu kwao.
  “Maneno mengi sana mtaani yanazungumzwa kwamba tutaenda kule kufuata magoli na sio kushinda lakini mimi pamoja na wachezaji wenzangu tunaona kama wanatutengenezea hasira ya kwenda kufanya maajabu ili kuwadhihirishia watu kuwa Yanga au Tanzania sasa ni nchi ya soka,”alisema.
  Yanga itavaana na timu hiyo ya Misri mjini Cairo ikiwa ni mechi ya kwanza ya Raundi ya kwanza ya michuano hiyo mikubwa kwa klabu barani Afrika.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KASEJA: CHONGENI, LAKINI TUTAISHIKISHA ADABU AL AHLY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top