• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 10, 2009

  CANNAVARO AVULIWA KIATU NA MCHEZAJI WA WHITECAPS


  Cannavaro wa kwanza kushoto akiwa na kocha Maximo na Mussa Mgosi na Jerry Tegete wa nyuma kabisa


  MSHAMBULIAJI wa klabu ya Vancouver Whitecaps ya Canada, James Marlon juzi alimzawadia kiatu beki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, baada ya kuona anachezea viatu duni kwenye mechi baina ya timu hizo, Uwanja wa taifa, Dar es Salaam.
  Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja Taifa, Dar es Salaam na Yanga kuibuka na ushindi wa 3-0, Marlon alimvulia viatu Cannavaro baada ya mchezo huo na kumuambia: “Utakuwa ukitumia hivi, unajua sana,”.
  Mshambuliaji huyo, kutoka visiwa vya Caribbean, nchini Saint Vincent na Grenadines, alisema Cannavaro ni beki mzuri ambaye anaweza kucheza popote duniani hata Ulaya.
  Kwa upande wake, Cannavaro alisema amefurahi kupewa zawadi hiyo. “Nashukuru, amenipa silaha bwana, hiki kiatu kikali sana, nitakitumia kupambana na Waarabu huko Cairo,”alisema huku akicheka beki huyo kutoka kisiwani Zanzibar.
  Mchezaji huyo anayesifika kwa desturi yake ya kujituma uwanjani, aliwahi pia kuvuliwa jezi na Samuel Eto’o, baada ya mechi dhidi ya Cameroon, akiichezea timu ya taifa ya Taifa, Taifa Stars mjini Younde kwenye mechi ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010 Afrika Kusini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CANNAVARO AVULIWA KIATU NA MCHEZAJI WA WHITECAPS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top