• HABARI MPYA

  Friday, March 27, 2009

  YANGA WAANZA KUSAKA FEDHA ZAO ZA GTV


  KLABU ya Yanga imelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kusaidia kupatikana kwa haki yao malipo yaliyotokana na udhamini wa televisheni ya kampuni ya GTV iliyositisha shughuli zake hapa nchini.
  Akizungumza mjini Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa Yanga, Imana Madega (PICHANI KUSHOTO) alisema mpaka sasa klabu hiyo haijui hatma ya suala hilo kutokana na TFF kuwa kimya.
  "Ule ulikuwa mkataba wa kisheria kati ya TFF na GTV si suala lilofanyika kienyeji sasa kwa nini tusipate haki yetu,"alihoji Madega.
  Alisema kuwa kwa kufuatana utaratibu wa kawaida wa kisheria pande zote zinazohusika katika suala hilo zinatakiwa kupata haki zake kulingana na taratibu za kuvunjia kwa mkataba.
  Hata hivyo jitihada za kumpata Katibu Mkuu wa TFF, Frederick Mwakalebela kuzungumzia suala hilo ziligonga ukuta baada ya kutopatika ofisini kwake huku simu yake ya mkononi ikiita bila kupokelewa.
  Televisheni ya GTV ambayo ilisitisha huduma zake hapa kwa kile kilichodaiwa kufilisika ilingia mkataba na TFF kwaajili ya kurusha baadhi ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na kutoa fedha za maandalizi kwa timu zote shiriki na zawadi kwa washindi watatu wa juu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA WAANZA KUSAKA FEDHA ZAO ZA GTV Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top