• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 30, 2009

  MGOSI ATAKIWA KUKABIDHI KADI ZA UANACHAMA TANGA

  Mgosi na Dalali


  WANACHAMA wa klabu ya Simba tawi la Tanga, wanamataka Mussa Hassan Mgosi aende kuwakakabidhi kadi za uanachama.
  Mgosi amekuwa swahiba wa wana Simba wote nchini baada ya kuchaguliwa kwenye kikosi cha nyota wa Michuano ya Ubingwa wa Mataifa Afrika (CHAN) iliyomalizika Februari mwaka huu mjini Ivory Coast, ambako Tanzania ilishiriki.
  Mgosi alikuwa mchezaji pekee wa Taifa Stars kuchaguliwa kwenye kikosi cha CHAN kama mchezaji wa akiba.
  Zaidi ya wanachama 1,000 wa matawi ya Simba mkoani Tanga, wanatarajiwa kukabidhiwa kadi zao za uanachama katika sherehe itakayofanyika Aprili 18, mwaka huu makao makuu ya matawi hayo eneo la barabara ya 16 kwenye ofisi za Tanga Line mjini Tanga.
  Mwenyekiti wa matawi ya Simba mkoani hapa, Mbwana Msumari alisema tayari wametuma maombi kwa uongozi wa klabu hiyo mjini Dar es salaam juu ya kuomba kwa Mwenyekiti Hassan Dalali ampeleke Mgosi kuwa mgeni rasmi atakayekabidhi kadi hizo kwa wanachama.
  "Tumemuomba Mwenyekiti, ili sherehe zetu zifane, aandae utaratibu wa kumfanya Mussa Mgosi kuwa mgeni rasmi katika sherehe zetu za kukabidhi kadi mpya za klabu yetu...Tunataka kumpa heshima mchezaji huyu kwa vile amekuwa akifanya vizuri kwenye timu yetu na ile ya Taifa, hii pia itatoa changamoto kwa wachezaji wengine," alisema Msumari.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MGOSI ATAKIWA KUKABIDHI KADI ZA UANACHAMA TANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top