• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 14, 2009

  CHEKA KUZIPIGA NA MRUSI  BONDIA Francis Cheka anatarajia kutetea mkanda wake wa ubingwa wa mabara unaotambuliwa na shirikisho la ngumi la UBO dhidi ya bondia Gani Spataev kutoka nchini Urusi, Mei 2 mjiniTanga.
  Akitangaza pambano hilo lilioandaliwa na Kampuni ya Best Man Promotion ya mkoani hapa, mkurugenzi wa kampuni hiyo, Zumo Makame alisema mpambano huo utakuwa wa raundi 12 katika uzito wa Middle.
  Makame alisema wameamua kumuandalia mpambano huo ,Cheka ili aweze kutetea mkanda huo wa UBO ili kumuepusha na hatari ya kupokonywa mkanda huo baada ya kukaa nao kwa muda mrefu tangu amchape Hassan Matumla kwa KO na kutwaa mkanda huo mapema mwaka jana.
  Alisema pamoja na kupanga kufanyika kwa mpambano huo mkoani Tanga kutokana na mkoa huo kuwa na chimbuko la mabondia, bado kampuni yake inaendelea kufanya tathmini ya mpambano huo kufanyika mkoani humo.
  Alisema rekodi nzuri ya bondia huyo wa Kirusi atakayekuja kucheza na Cheka anayetokea katika Jimbo la Kyrgysztan ndiyo iliyomvutia kumleta nchini kwa kushirikiana na Shirikisho la Ngumi la PST na kuwataka wakazi wa Morogoro na mikoa ya jirani kumpa ushirikiano katika kipindi hiki cha maandalizi.
  Cheka anayeshikilia mkanda wa ubingwa wa mabara UBO na ubingwa wa dunia ICB alisema pamoja na uzuri wa mabondia kutoka Russia ana uhakika wa kushinda mpambano huo kutokana na maandalizi atakayofanya.
  "Nimeshacheza na Mrusi mwaka jana kule Uingereza na alinipiga kwa pointi, najua wana nguvu na wavumilivu, lakini nitahakikisha nafanya mazoezi ya kutosha ili nishinde mpambano huo,"alisema.
  Kocha wa Cheka ,Abdallah Saleh 'Komando'alisema atamuongezea mazoezi bondia wake ili aweze kuibuka na ushindi dhidi ya bondia huyo na kuwaishukuru Kampuni ya Best Man kwa kumuandalia mpamano huo bondia huyo kwani utaendelea kumpa uzoefu.
  Hili ni pambano la tatu kwa Cheka kuandaliwa na Kampuni ya Best Man Promotion ya mjini hapa ambapo katika mapambano yaliyopita, Cheka aliibuka na ushindi ,akianzia kwa Richard Onyango kutoka Kenya na Rashid
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHEKA KUZIPIGA NA MRUSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top