• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 14, 2009

  PHIRI: MABEKI WANGU BUTU SIMBA


  KOCHA wa Simba, Patrick Phiri (pichani kulia) amesema kufanya vibaya kwa wachezaji wake kumetokana na mabeki wa timu yake kukosa umakini na kupoteza pasi nyingi na kuruhusu wapinzani wao kuwasoma mapema katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Vancover uliofanyika katika Uwanja wa Taifa.
  Katika mchezo huo, Simba walishindwa kuonyesha makali yao baada ya kuruhusu magoli 2-1, hivyo kocha huyo kulaumu safu ya mabeki kwa kukosa umakini na kusababisha wapinzani wao kutumia mwanya huo kuwamaliza.
  Akizungumza na Mwananchi jana kocha huyo alisema bado ana matumaini makubwa na kikosi chake na amesema kiko imara ili kilichowaangusha katika mchezo wa juzi ni mabeki wake kushindwa kuwa makini katika kutambua mbinu za maadui zao.
  "Simba ni timu nzuri na ina wachezaji ambao wana kiwango kizuri katika nafasi zao na katika mchezo wa juzi safu ya mabeki ndio ilisababisha tukapoteza mchezo huo lakini bado kikosi changu kiko imara na kwa sasa tunajipanga kwa ajili ya kumalizia mzunguko huo wa pili wa ligi kuu ulioanza,"alisema.
  Aidha, kocha huyo amewataka wachezaji wake kujituma zaidi katika mazoezi na kuwa na ushirikiano wa kutosha baina yao na viongozi wao pamoja na wao wenyewe kwani hiyo ni moja ya kuwaweka katika nafasi nzuri ya kushinda katika mechi zilizosalia.
  Simba ina point 24 huku watani wao, Yanga wakiongoza msimamo wa ligi hiyo kwa kuwa na point 42 wakifuatiwa na JKT Ruvu na Polisi Dodoma wakiwa na hatihati ya kushuka daraja msimu ujao kwa kushika mkiwa
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PHIRI: MABEKI WANGU BUTU SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top