• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 07, 2009

  PHIRI AKATAA KUNUNUA KESI YA MAXIMO NA BOBAN


  KOCHA Patrick Phiri wa Simba amesema hana matatizo na mchezaji wake, Haruna Moshi (KUSHOTO) anayedaiwa kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu akiwa na timu ya taifa, Taifa Stars.
  Phiri alikuwa ameulizwa kama ana maoni yoyote kuhusiana na utovu wa nidhamu unaodaiwa kufanywa na mchezaji huyo, wakati kikosi cha Stars kikiwa mashindanoni Ivory Coast.
  “Sijapata taarifa yo yote ya maandishi wala mdomo kuhusu kilichotokea Ivory Coast. Lakini hata kama ningepata taarifa, mimi siwezi kumfanya chochote kwa sababu sijui mazingira yalikuwaje.
  “Sikuona vitendo vya utovu wa nidhamu anavyodaiwa kufanya, sikuwepo kule. Angekuwa amekwenda na Simba, sawa. Kama kuna chochote cha kufanywa basi kinatakiwa kifanywe katika timu ya taifa,” alisema kocha huyo.
  Kuhusu jinsi anavyomuona mchezaji huyo kitabia, alisema kwa upande wake haoni tatizo lolote, kwani ni mchezaji mwenye kipaji, anayejituma na mwenye nidhamu ndani na nje ya uwanja.
  Alisema utovu wa nidhamu ni neno la jumla kwa kuwa lina maana pana ambayo kila mmoja ana tafsiri yake. “Kwa hiyo siwezi kujua ni utovu gani wa nidhamu, mtu mwingine anaweza kuonekana hana nidhamu kwa kucheka tu,” alisema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PHIRI AKATAA KUNUNUA KESI YA MAXIMO NA BOBAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top