• HABARI MPYA

  Friday, March 20, 2009

  MRENO AJA KUINOA AFRICAN LYON  MRENO Eduardo Fillipe Arojja Almeida, aliyezaliwa mwaka 1978 ndiye atakuwa kocha wa klabu ya African Lyon, iliyopanda Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania kwa ajili ya msimu ujao, imeelezwa.
  Mehdi Rehmtulla, bosi wa klabu hiyo yenye mipango ya kuleta mabadiliko makubwa katika soka ya nchi hii, aliiambia DIMBA kwamba mambo yanaendelea vizuri kuelekea kwenye mchakato wa kufanya vitu adimu katika kandanda nchi hii.
  “Huyu jamaa ni bwana mdogo sana, amesoma sana, anaijua soka, hakuna kocha kama huyu nchi hii, yeye anakuja hapa, lengo kubwa ni kiutengeneza wasifu wake.
  Anataka afanye mambo makubwa, na kikubwa alichofurahi timu yangu ni changa,”alisema Mehdi. (kulia na mmilik wa METL) inayoimiliki African Lyon, Mohamed Dewji mbunge wa Singida mjini)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MRENO AJA KUINOA AFRICAN LYON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top