• HABARI MPYA

    Saturday, March 14, 2009

    MWANAMKE AWA RAIS BFT


    MWANAMAMA Johan Minja (pichani juu) leo amechaguliwa kuwa rais mpya wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Nchini BFT katika uchaguzi uliofanyika kwenye Ukumbi wa Baraza la Maaskofu, Kurasini mjini Dar es Salaam.
    Johan aliibuka mshindi baada ya kumbwaga, Hezron Kigondo kwa kura 60 kwa 42. Awali wagombea hao waligongana kwa kura 54 kila mmoja na ndipo uchaguzi uliporudiwa na Johan kuibuka kinara.
    Nafasi ya Makamu Mwenyekiti ilikwenda kwa Michael Changarawe aliyepata kura 64 na kuwashinda, Remmy Ngabo na Said Mgawe ambaye alijitoa awali.
    Andrew Muhonja aliibuka mweka hazina kwa kura 82 na kumshinda Lucas Michael, hadi tunakwenda mitamboni matokeo mengine yalikuwa yakiendelea kutangazwa.
    Katika uchaguzi huo ambao wapiga kura 124 walishiriki, awali mgombea nafasi ya urais, Shomari Kimbau alitolewa katika kinyang’anyiro hicho.
    Kimbau alitolewa baada ya wajumbe wa mkutano kudai kwamba katiba ya BFT hairuhusu watu wanaojihusisha na ngumi za kulipwa kugombea uongozi BFT.
    Uchaguzi huo ulifanyika kufuatia kung’atuka kwa kamati nzima ya utendaji ya BFT iliyokuwa ikiongozwa na Shaaban Mintanga ambaye anatuhumiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MWANAMKE AWA RAIS BFT Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top